TANGAZO


Thursday, February 27, 2014

Mama ajifungulia barabarani New York


Cian na mkewe tayari wana watoto wawili
Mwanamke mmoja raia wa Uingereza amejifungulia katika barabara moja mjini New Yorkakiwa njiani kuelekea hospitali kutokana na uchungu wa uzazi.
Polly McCourt, mwenye umri wa miaka 39,aliondoka nyumbani kwake katika mtaa wa East Side siku ya jumatatu na kujaribu kukodisha taxi hadi alipogundua kuwa mwanawe asingeweza kusubiri.
Mama na mtoto walikuwa salama walipofikishwa hospitalini.Wapita njia walimpa mama huyo koti na vitambaa walivyokuwa navyo kumfunika mwanawe hadi wahudumu walipofika kumsaidia na kumpeleka hospitaliini.
"alipiga mayowe akisema Mungu wangu mtoto wangu yuaja ,'' alisema shahidi mmoja.
Na niliweza kuona kichwa cha mtoto. Tulipomlaza mama chini kumsaidia, mtoto akawa tayari ametoka.''
Bi McCourt, anayetoka nchini Uingereza alijifungua mwanawe kando ya barabara.
Mama huyo alionekana akitabasamu alipoingia katika gari la ambulensi na kupelekwa katika hospitali ya Lennox Hill mjini New York.
Mumewe mama huyo alikuwa amekwama barabarani kutokana na msongamano wa magari alipopata simu kutoka kwa mkewe.
Wawili hao tayari wana watoto wengine wawili, Conor mwenye umri wa miaka sita na Adele mwenye umri wa miaka minne kulingana na jarida la New York Daily News.
Inaarifiwa walihamia mjini New York miaka minne iliyopita kutoka Dublin nchini Ireland.

No comments:

Post a Comment