TANGAZO


Sunday, February 23, 2014

Malema sasa azindua manifesto ya chama


Julius Malema akiwahutubia wafuasi wa chama chake

Kiongozi wa Upinzani mwenye utata nchini Afrika ya kusini Julius Malema amezindua manifesto ya chama chake mbele ya umati mkubwa wa wafuasi elfu 30 katika uwanja mmoja uliopo mji wa viungani mwa Johannesburg.
kiongozi huyo wa zamani wa vijana katika chama cha ANC ambaye kwa sasa anakiongozi chama cha Economic Freedom Front EFF amesisitiza wito wake wa kuyanyakua mashamba yanayomilikiwa na wazungu nchini humo mbali na kutaka migodi yote kuwa mali ya kitaifa.
Chama cha EFF kiliundwa mwaka 2012 baada ya Malema na washirika wake kufukuzwa katika chama cha ANC aliposhtumu uongozi wa chama hicho.
Hatahivyo waandishi wanasema kuwa ANC ina nguvu ya kushinda uchaguzi ujao wa mwezi Mei.

No comments:

Post a Comment