TANGAZO


Friday, February 21, 2014

Ghana yatoa heshima kwa Komla Dumor

Komla na aliyekuwa waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai
Hafla mabli mbali za siku tatu kumuenzi aliyekuwa mtangazaji wa BBC Komla Dumor-aliyefariki ghafla mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 41,zitaanza leo nchini Ghana kabla ya maizko yake.
Baada ya kifo chake,rambirambi zilitolewa kutoka kote dunia na rais wa Ghana,John Mahama,alisema kuwa Ghana imempoteza balozi.
Umati mkubwa unatarajiwa kuhudhuria.Kama ilivyo desturi nchini Ghana,hafla ya mazishi yake itachukua muda wa siku tatu ikianza na misa ya kuomboleza katika kanisa la Accra Roman Catholic cathedral ambapo wananchi wataruhusiwa kutazama mwili wake.
Jumamosi,wasifu wake utasomwa ukisifia yale aliyofanya nchini mwake. Ibada hiyo itafanyika katika uwanja wa Ikulu ya Ghana Ikifuatwa na ibada ya mazishi itakayohusisha familia yake pekee.
Komla Dumor alikuwa mtangazaji maarufu katika stesheni moja ya redio nchi Ghana kabla ya kujiunga na BBC miaka saba iliyopita na aliweza kufahamika kama mtangazaji wa redio na televisheni mwenye haiba kubwa duniani kote.
Katika kazi yake alipenda kuonyesha watazamaji wake kuhusu bara la Afrika na kuwawezesha kuelewa Afrika kwa kina. Kufuatia kifo chake,aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa,Kofi Annan alisema kuwa Afrika imempoteza mmoja wa talanta zake chipukizi.
Aliongeza kwamba, Komla Dumor alikuwa mtangazaji mwenye kupeana motisha aliyedhamiria kuchimbua ukweli na kutangaza ukweli kila wakati.
Maneno haya yalilingana na yale yaliyotolewa na wabunge wa Ghana siku ya Alhamisi. Katika ibada hiyo,mbunge mmoja alitaja kuwa serikali ilikuwa imekubali kuipa jina barabara moja jijini kama ishara ya kumkumbuka.

No comments:

Post a Comment