TANGAZO


Tuesday, February 25, 2014

Gazeti lawataja 'mashoga' Uganda



Rais Museveni amepitisha sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja Uganda

Gazeti moja la udaku nchini Uganda la Red Pepper limechapisha orodha ya majina 200 wanayodai ni ya wale wanaojihusisha na mapenzi ya watu wa jinsia moja.
Orodha hiyo inakuja siku moja tu baada ya Rais Museveni kutia saini sheria imepenkezayo adhabu kali kwa wanaojihusisha na kuendeleza tabia hiyo.
Baadhi ya majina yaliyomo kwenye gazeti hilo liitwalo Red Pepper ni watu ambao hawajatangaza wazi iwapo wanashiriki mapenzi ya jinsia moja au la.
Sheria hiyo mpya inawadhibu kifungo cha maisha wanaoshiriki ushoga na kupiga marufuku jambo lolote linalonadi tabia hiyo.
Marekani ilikuwa imeionya Uganda kuwa uhusiano wa nchi hiyo na mataifa ya magharibi utatatizika na sasa Denmark, Norway na Uholanzi imetangaza itasitisha misaada kwa Uganda.

No comments:

Post a Comment