Mwanaharakati Ulaya
Kamishna wa bara ulaya anayesimamia maswala ya ndani ya bara
hilo ameonya kuhusu viwango vya juu vya ufisadi miongoni mwa nchi wanachama wa
bara hilo.
Katika taarifa aliyoandika katika gazeti moja la nchini Sweden,Cecila
Malmstrom amesema kuwa Ufisadi unaondoa uaminifu katika taasisi nyingi za
kidemkrasia,kuharibu uchumi na kujenga mazingira yanayokuza uhalifu.Amesema kuwa ufisadi umesababisha gharama ya hadi dola millioni 160 kwa mwaka.
Amesema kuwa tatizo hilo limekuwa likitokea katika mataifa tofauti na kwamba hakuna ambalo halijaathirika .
No comments:
Post a Comment