Mahakama maalum ya Kimataifa ya Rwanda- ICTR imefutilia mbali kesi dhidi ya maafisa waandamizi wawili watuhumiwa wa mauaji ya kimbari Rwanda.
Uamuzi huu umetolewa katika kesi yao ya rufaa.
Aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi Augustin Ndindiliyimana, ameelezewa kama mmoja wa watu wa ngazi ya juu waliohukumiwa na mahakama hiyo inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa.Walishitakiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994, ambayo inakadiriwa watu laki nane walipoteza maisha.
Afisa wa pili, Francois-Xavier Nzuwonemeye alikuwa kamanda msomi wa kikosi cha jeshi.
Mahakama ya ICTR pia imepunguza muda wa kifungo cha afisa wa tatu.
Hata hivyo uamuzi kuhusu rufaa ya mkuu wa zamani wa Jeshi Augustin Bizimungu haujatangazwa bado.
No comments:
Post a Comment