TANGAZO


Thursday, January 2, 2014

Zitto Kabwe aibwaga Chadema Mahakama Kuu


Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe (kulia), akitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam leo, ambapo aliwasilisha ombi la pingamizi la yeye kutokujadiliwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho, kinachotarajiwa kufanyika kesho, hadi rufaa yake ya kupinga kuenguliwa wadhifa huo itakapotolewa kwenye Baraza Kuu la chama hicho. Kushoto ni Wakili wa Zitto, Albert Msando. Mahakama Kuu imekubaliana na Zitto kuhusu kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kinachotarajiwa kufanyika kesho kutomjadili kwa namna yoyote. (Picha zote na Kamda wa Matuko blog)
Zitto Kabwe akiingia Mahakama Kuu, Dar es Salaam leo.
Wanasheria wa Chadema, Tundu Lisu (kushoto) na Peter Kibatala waliofika kupinga hoja hiyo mahakamani.
Tundu Lisu na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakijadiliana jambo wakati wakisubiri uamuzi wa mahakama
Zitto Kabwe akiwa na wakili wake, Msando wakiwasiliana na marafiki zao walipokuwa wakisubiri uamuzi wa Mahakama, ambapo Zitto aliibuka kidedea kwa pingamizi lake kukubaliwa hivyo, kikao cha Kamati Kuu kinachofanyika kesho kuzuiwa  kumjadili kwa namna yoyote Zitto.

No comments:

Post a Comment