Jumuia ya kimataifa imelaani vikali shambulio la kujitolea
mhanga kwenye mkahawa wa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, ambao liliuwa watu kama
21 - wengi wao wageni.
Waziri wa mambo ya ndani wa Afghanistan, Mohammad Omar Daudzai, amesema
maafisa kadha wa serikali ya mitaa wamesimamishwa kazi na uchunguzi
unafanywa.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani shambulio hilo kuwa kitendo cha kutisha.
Mkahawa huo uko katika mtaa wa Kabul wa watu wanaojiweza na ukipendwa na wageni na maafisa wa serikali.
Taliban wamesema wamehusika na shambulio hilo.
Wageni 13 kutoka Marekani, Canada, Urusi, Libnan na Uingereza wameuwawa - na wengine ni raia wa Afghanistan.
Taarifa zinasema kuwa mshambuliaji alijilipua kwenye mlango wa mkahawa.
Baada ya mlipuko watu wawili waliwafyatulia risasi wateja
No comments:
Post a Comment