Serikali ya Sudan Kusini inasema kuwa jeshi lake limekomboa mji
wa Bor kutoka kwa waasi wa Riek Machar.
Msemaji wa jeshi Philip Aguer, amesema kuwa wanajeshi wa Sudan Kusini
waliwashinda zaidi ya waasi, elfu kumi na tano wanaomtii Machar ambaye alikuwa
makamu wa Rais wa zamani wa Rais Salva Kiir kabla ya wawili hao
kutofautiana.Bwana Aguer, ameelezea kwamba hatua ya jeshi kuukomboa mji huo, imeondoa wasiwasi wa waasi hao kuufikia mji mkuu Juba ambao uko Kusini mwa Bor.
Mji wa Bor umetekwa mara kadhaa tangu vita vya Sudan Kusini kuanza na kudumu kwa mwezi mmoja sasa.
Mwandishi wa BBC mjini Juba anasema kuwa jeshi sasa litaangazia zaidi kuukomboa mji wa Malakal ambao uko Kaskazini mwa nchi unaodhibitiwa kwa sasa na waasi katika juhudi za kuikomboa miji yote inayodhibitwa na waasi.
No comments:
Post a Comment