Baadhi ya Wajumbe Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, wakiwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, walipofika kwa ajili ya kujadili na kutathmani utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) katika Halmashauri ya Kibaha. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya Wajumbe Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii na Maofisa wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, wakiwa nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, wakijiandaa kuelekea Ofisi za Halmashauri ya Mji wa Kibaha kwa ajili ya kujadili na kutathmani utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) katika halmashauri hiyo.
Wajumbe Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii na Maofisa wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, wakiwa kwenye Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Kibaha kwa ajili ya kupata taarifa ya utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) katika halmashauri hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Jenifa Omolo, akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) kwa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, ilipofika ofisini kwake kwa ajili ya kupata taarifa hiyo pamoja na kwenda kuvitembele vikundi vinavyofahiliwa na mfuko huo.
Wajumbe Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii na Maofisa wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Jenifa Omolo (hayupo pichani), alipokuwa akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF), ofisini kwake jana.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii na Maofisa wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Jenifa Omolo (hayupo pichani), kuhusu Utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF), ofisini kwake jana.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Jenifa Omolo, akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii (hawapo pichani), walipofika ofisini kwake kwa ajili ya kupata taarifa hiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Dk. Maua Abeid Daftari, akisaini kitabu cha wageni, alipofika na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, Ofisi ya Kata ya Mwendapole, Visiga mkoani Pwani jana.
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, wakisaini kitabu cha wageni, walipofika ofisi ya Kata hiyo, jana.
Wanakikundi cha Wajasiriamali wanawake cha Tunda cha Mwendapole, Visiga, mkoani Pwani, wakiimba na kufurahi wakati wakiwapokea Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, walipowatembelea kwenye ofisi yao, kuangalia miradi na kutathmini maendeleo yao kutokana na ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) kwa vikundi mbalimbali vya wanawake wajasiriamali katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha, mkoani Pwani.
Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Kapteni John Komba, Mbunge wa Mbinga Magharibi, akizungumza na wajasiriamali wa kikundi hicho cha Tunda kilichopo Mwendapole, Visiga, mkoani Pwani jana.
Mjumbe wa kamati hiyo ya Bunge, Mbunge wa Lindi Mjini, Salum Barwani, akizungumza na wajasiriamali wa kikundi hicho.
Wanakikundi cha Tunda cha Visiga, Kibaha mkoani Pwani wakisikiliza maelezo ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, wakati walipofika kuangalia na kutathmini maendeleo yao kutokana na ufadhili wa mfuko huo.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Dk. Maua Abeid Daftari na Mkurugenzi wa Halimashauri ya Mji wa Kibaha, wakisikiliza risala ya wajasiriamali wanawake wa kikundi cha Tunda kilichopo Mwendapole, Kibaha, mkoani Pwani.
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, wakisikiliza risala ya kikundi hicho, iliyokuwa ikisomwa na Mwenyekiti wa kundi hicho.
Mwenyekiti wa kundi hicho, akisoma risala ya kikundi mbele ya wajumbe wa kamati hiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Dk. Maua Abeid Daftari, akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, Mbunge wa Manyovu Kigoma, Albert Obama, Kapteni John Komba wa Mbinga Magharibi na Salum Barwan wa Lindi Mjini,
kwenye mkutano huo.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Dk. Maua Abeid Daftari, akizungumza na kikundi cha wajasiriamali wanawake hao wa kikundi cha Tunda kilichopo Mwendapole, Kibaha, mkoani Pwani.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Dk.Maua Abeid Daftari, akizungumza na kikundi cha wajasiriamali wanawake wa kikundi cha Tunda kilichopo Mwendapole, Kibaha, mkoani Pwani, kuhusu tathmani ya utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF), wakati walipotembelea Halmashauri ya Kibaha, kufuatilia utekelezaji wa mfuko huo jana.
Mjumbe wa Kamati hiyo, Mbunge wa Manyovu Kigoma, Albert Obama, akizungumza na wanakikundi hicho.
Wajumbe wa Kamati hiyo, wakiangalia bidhaa zinazozalishwa na kikundi hicho cha Tunda.
Wajumbe wa Kamati hiyo, wakiangalia na wengine kununua bidhaa zinazozalishwa na kikundi hicho cha Tunda.
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, wakiagana na baadhi ya viongozi wa Mtaa wa Mwenapole.
Wajasiriamali hao, wakiwaaga wanakamati hiyo, kwa nyimbo mbalimbali, wakati wakiondoka katika maeneo hayo.
Wanavikundi vya wa Amani na Tumaini, wakiwa katika mkutano na kamati hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Jenifa Omolo, akitoa maelezo kabla ya kumkaribisha Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Dk. Maua Abeid Daftari (kulia), wakati walipofika Visiga Miwaleni kukutana na vikundi vya akinamama wajasiriamali, vya Amani na Upendo kuzungumza nao, kujadili na kutathmani utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF), katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha, mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa kikundi cha Amani, akisoma risala kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo kwenye miradi yao ya ujasiriamali.
Wanavikundi vya Amani na Upendo wakiwa kwenye mkutano huo na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, walipofika kwa ajili ya kujadiliana nao, kuthmini na kuangalia maendeleo ya miradi yao, inayofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya wanawake (WDF) katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha, mkoani Pwani.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Salum Barwan, Mbunge wa Lindi Mjini, akizungumza na wanavikundi hao.
Wjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, wakiangalia bidhaa zinazozalishwa na vikundi hivyo, pia kununua bidhaa hizo ili kuwatia hamasa za katika kuendeleza miradi yao hiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Dk. Maua Abeid Daftari, Mbunge wa Viti Maalum kutoka Kaskazini Pemba, akitoa majumuisho ya ziara yao katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha, mkoani Pwani, wakati walipokuwa wakihitimisha ziara yao hiyo jana.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Dk. Maua Abeid Daftari, akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, wakijipumzisha mara baada ya kumaliza ziara yao hiyo jana.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Dk. Maua Abeid Daftari, akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara yao hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Meshack Ndaskoi.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mbunge wa Manyovu Kigoma, Albert Obama, akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara yao hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Jenifa Omolo, akizungumza wakati wa majumuisho hayo.
No comments:
Post a Comment