Kamanda Mkadam akionesha moja ya Silaha aina ya SMG ambayo ilikuwa haina magazine waliokuwa wakiitumia watuhumiwa wa uhalifu katika maeneo ya Raha Leo na kuitupa katika eneo la msikiti wa Muembe Shauri wakati wakikimbia.
Kamanda Mkadam akiwaonesha waandishi moja ya silaha aina ya Gobole,waliofanikiwa Jeshi la Polisi kumkamata mtuhumiwa wakati akijiandaa kwenda kufanya uhalifu maeneo ya Mtoni.
Kamanda Mkadam akionesha bastola iliyotumia katika uhalifu wa kumpora fedha mfanyabiashara katika maeneo ya rahaleo Zanzibar ikiwa na risasi zake kamili, ilihusika katika tukio hilo.
Kamanda Mkadam akisoma taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu bastola iliyotumiwa katika uhalifu wa kumpora fedha mfanyabiashara katika maeneo ya rahaleo Zanzibar ikiwa na risasi zake kamili, ilihusika katika tukio hilo.
Sehemu ya Silaha waliokuwa wakiitumia watuhumiwa wa uhalifu katika maeneo ya Raha Leo na kuitupa katika eneo la msikiti wa Muembe Shauri wakati wakikimbia.
Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa inayotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamanda Mkadam Khamis Mkadam, kuhusiana na uhalifu uliofanyika mwanzo mwa wiki hii katika maeneo ya Rahaleo na kumpora fedha shilingi milioni kumi na moja katika tukio hilo na polisi kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao, kwa ushirikiano wa Wananchi wa Kwahani.
No comments:
Post a Comment