Hivi ndivyo utakavyokuwa Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, unaojengwa katika Viwanja vya Michezani, mjini Unguja.
Hatua ya mwazo ya ujenzi wa mnara huo, inavyoendelea na ujenzi wake unaojengwa na Kampuni ya CRJE ya China.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mshauri Ujenzi wa Mnara huo, Habibu Nuru wa Kampuni ya Hab Consult, alipofika kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mnara huo, unaojengwa katika maeneo ya Michezani Kisonge, mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa pazia kuashiria kuweka jiwe la msingi la Mnara wa kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wengine wakifurahia uwekaji wa jiwe hilo la Msingi.
No comments:
Post a Comment