TANGAZO


Wednesday, January 8, 2014

Rais wa Zanzibar Dk. Shein afungua Taasisi ya Sitti Bit Saad mjini Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Viongozi na wananchi wakati alipozindua Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika  ukumbi wa Salama Hall, Bwawani Hotel Mjini Unguja jana, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisoma maandishi  yanayosomeka "TAASISI YA MWANAHARAKATI BIBI: SITI BINTI SAAD" mara baada ya kufanya izinduzi wa Taasisi hiyo jana katika  ukumbi wa Salama Hall, Bwawani Hotel Mjini Unguja, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimakabidhi Picha ya Bibi Siti Binti Saad, Nasib Amour, kwa niaba ya Zanlink, iliyonadishwa na kufikia bei ya Tsh Laki Tano, pia zanlink itawaunganishia Mtandao wa Internet kwa mwaka mmoja, wenye gharama ya Dola Elfu moja na Nusu,wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika  ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimakabidhi Picha ya Bibi Siti Binti Saad, Mbunge wa Jimbo la Mpendae Salum Turky,aliyoinunua kwa mnada kwa bei ya Tsh Millioni Moja, wakati wa uzinduzi wa
Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika  ukumbi wa
Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya
shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimakabidhi Picha ya Bibi Siti Binti Saad,Prof Martin Mhando, mwanakamati katika taasisi, iliyonadihswa kwa bei ya Tsh laki mbili na Hamsini Elfu,wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika  ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar .
Kikundi cha Taarab asilia cha Rahatu zamani, kikitoa burudani yao wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Bnti Saad,katika  ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar (pichani), Muharami Mohamed, kitukuu akiimba moja ya nyimbo za marehemu Bibi Siti Binti Saad.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati), akiwa katika picha ya pamoja iliyowajumuisha Viongozi Wakuu wa Serikali na wasanii wa
Kikundi cha Taarab asilia cha Rahatu zamani, wakati wa uzinduzi
wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Bnti Saad, katika  ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati), akiwa katika picha ya pamoja iliyowajumuisha Viongozi wakuu wa Serikali na wana kamati wa  uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Bnti Saad, katika  ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, alipohudhuria katika uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad, katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel jana, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 50 ya mapinduzi Ya zanzibar (katikati), Bibi Nasra  Mohamed Halal Mwenyekiti wa Taasisi.
Watoto wakiimba nyimbo mbali mbali za michezo  ya kizamani ikiwemo nyimbo ya ukuti,wakati wa  Uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad, ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi ni miongoni mwa Wananchi waliohuduria katika uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika  ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,taasisi hiyo iliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, ikiwa  ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Wananchi waliohuduria katika uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika  ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akitoa hutuba yake ikiwa  ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar. 
Wananchi kutoka mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja walihuduria katika uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika  ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel (pichani) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akihutubia jana, 
ikiwa  ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi 
Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,(kushoto) akiwa mlezi wa  Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad akifuatiwa na Mwenyekiti wake Bibi Nasra  Mohamed Halal, wengine kulia Makamo wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo  Said Ali Mbarouk, wakiwa katika Uzinduzi wa Taasisi hiyo iliyozinduliwa jana katika  ukumbi
wa Salama Hall Bwawani Hote, ikiwa  ni sehemu ya shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Profesa Laura Fair, aliyefanya utafiti na kutunga kitabu cha wa mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad,akizindua kitabu hicho wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya mwanaharakati huyo iliofanya jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shei,(hayupopichani) katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel mjini Unguja,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Historia ya Harakati za wanawake iliyotolewa na Dk. Amina Ameir,mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni
sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na kumpongeza Dk.Amina Ameir, baada ya kutoa Historia ya Harakati za wanawake katika uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika  ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pamoja na Viongozi wengine wakiangalia picha ya Bibi Siti Binti Saad, iliyokuwa ikipigwa mnada katika uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika  ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saa,Bibi Nasra Mohamed Hilal,alipomkaribisha mlezi wa taasisi hiyo Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,kuzungumza machache ili nae amkaribishe mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kutoa hutuba yake na kuizindua rasmi katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimshukuru Muharami Mohamed,Kitukuu cha Bibi Siti Bnti Saad,baada ya kumpa zawadi ya kofia aliyoivaa, wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika  ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar. 
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,(akiyesimama) akiwa mlezi wa  Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad,akimkaribisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, kuizindua taasisi hiyo katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Viongozi na wananchi wakati alipozindua Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika  ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.


Na Said Ameir,Zanzibar                                                                    08Januari, 2014
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa wito kwa wasanii chipukizi kujifunza zaidi kutoka kwa wasanii wa zamani ili kuimarisha vipaji vyao na kutoa mchango zaidi katika maendeleo ya sanaa nchini.
 
Kauli hiyo ameitoa jana usiku wakati wa ukizinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Siti Bint Saad uliofanyika katika hoteli ya Bwawani mjini Unguja.
 
Afafanua kuwa yapo mengi wasanii hao wa zamani waliyazingatia katika kazi zao za usanii na ndio maana hadi sasa wanakumbukwa na kazi zao zinazidi kupendwa hivyo wasanii chipukizi hasa wa muziki wa taarab hawana budi kujifunza kutoka kwa wasanii hao.
 
Alisema ubunifu na nidhamu katika sanaa ikiwemo muziki wa taarab ni jambo la kuzingatiwa kwa kuwa taarab ni muziki wenye kuburudisha na kukonga nyoyo za wanausikiliza kwa utulivu na kucheza kistaarabu.
 
Kwa hiyo aliwapongeza waanzilishi wa Taasisi ya Mwanaharakati Siti Bint Saad kwa kuanzisha taasisi hiyo ya aina yake kushughulikia fani ya mila, utamaduni na ubunifu.
 
Alibanisha kuwa ni hatua muafaka Taasisi hiyo kumtumia msanii huyo kuwa kigezo cha mafanikio katika harakati za wanawake za kujileta maendeleo na kwamba mafanikio yake yatatumika kama kielelezo cha kushajiisha wanawake humu nchini kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.
 
Hivyo aliieleza hadhara iliyoshiriki uzinduzi huo kuwa wana wajibu wa kuzingatia mafunzo yanayopatikana katika maisha na kazi za masanii Siti Bint Saad huku akihimiza kufanywa utafiti zaidi wa kazi za msanii huyo ambaye alikuwa na sifa za pekee kwa kuweza kuimba, kutunga na kupiga ala za muziki.   
 
Katika hotuba yake hiyo ambayo wakati mwingine alinukuu nyimbo za msanii huyo na kuvuta hisia za washiriki Dk. Shein alisema Serikali itaendelea kuwaenzi wasanii wote walioiletea sifa Zanzibar na kuwahakikishia kuwa jitihada zinafanywa za kuzihifadhi kazi zao kwa faida ya sasa na baadae sambamba na kuhakikisha kuwa wasanii hao wanafaidika na jasho la kazi zao.
 
Wakati huo huo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi alimueleza Siti Bint Saad kuwa msanii aliyekuwa amekamilika kisanii akiwa mahiri, gwiiji na mwenye uwezo mkubwa kughani mashairi na matumizi ya lugha ya Kiswahili, Kiarabu na Kihindi.
Mzee Mwinyi ambaye alibahatika kumjua na kumuona msaanii huyo katika uhai wake akiwa katika shughuli zake za sanaa alisema msanii huyo hakuwa gwiji katika uimbaji wa nyimbo za mapenzi tu bali pia katika nyimbo za kizalendo na kunukuu baadhi ya nyimbo zake ambazo aliwahi kuziimba.  
  
Akizungumzia shughuli za Taasisi hiyo Profesa Martin Mhando alieleza kuwa lengo kubwa la taasisi ni kuzienzi kazi za msanii huyo miongoni mwake kwa kuzitafuta na kuzihifadhi kazi zake, kuanzisha tuzo ya Siti Bint Saad kwa wasanii na kutenga siku ya Usiku wa Siti Bint Saad kila mwaka.
 
Kuhusu wasifu wa msanii huyo maarufu wa Taarab uliosomwa na Dk. Amina Ameir Issa ulieleza kuwa Siti Bint Saad alikuwa mwanaharakati aliyepigania haki na heshma ya watu wanyonge wa Zanzibar.
 
Alieleza kuwa Siti Bint Saad aliwakilisha kilio cha watu wa ‘ng’ambo’(nje ya mji) ambapo katika nyimbo zake alieleza maisha na matukio ya kila siku ya watu masikini waliokuwa wakiishi maeneo hayo na ilisadifu kuitwa ‘sauti ya watu wa ng’ambo’.
 
Aliongeza kuwa wakati taarab ilipokuwa mashuhuri miongoni mwa koo za kifalme na vijana matajiri wa kiarabu mwanzoni mwa karne ya ishirini Siti Bint Saad aliuchukua muziku wa taarab kutoka huko hadi kwa wananchi maeneo ya ‘ng’ambo’ ambapo alichangia kuanzishwa vikundi mbalimbali vya muziki huo.   
 
Kuhusu mchango wake katika kuendeleza lugha ya kiswahili Dk. Amina alisema msaani huyo ambaye alikuwa wa kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki kurekedi santuri mwaka 1928 alitoa mchango mkubwa kwa kuwa kuenea kwa muziki wa taarab na hasa kusambazwa kwa rekodi zake zilikipeleka kiswahili mbali hadi nchni Kongo wakati huo ikitawaliwa na Wabelgiji.  
Naye Mwanahistoria mtafiti Profesa Laura Fair kutoka Marekani alielezea maudhuni ya kitabu chake kuhusu historia na harakati za Siti Bint Saad pamoja na kikundi chake cha taarab kilivyopinga ukandamizaji wa wananchi.
Alihimiza umuhimu wa watu kujua na kuenzi historia zao na kutoa wito kwa wananchi wa Zanzibar kuweka kumbukumbu za maisha vyema kwa  faida ya sasa na vizazi vijavyo.
Hafla hiyo ambayo iliyohudhuriwa na watu mashuhuri na viongozi  mbalimbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi ilipambwa na muziki wa taarab asilia na waimbaji akiwemo kirembwe cha msanii Siti Bint Saad aitwae Bi. Muharami Mohamed.

No comments:

Post a Comment