TANGAZO


Sunday, January 12, 2014

Rais wa Zanzibar, Dk. Shein aendelea kutunuku nishani ya Mapinduzi


Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Makamo wa Kwanza wa Rais  wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja aliposhiriki katika hafla ya kutunuku Nishani ya Mapinduzi, katika shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Fatma Karume akisalimiana na Makamo wa Kwanza wa Rais  wa Zanzibar Maalim Seif Sharif katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja aliposhiriki katika hafla ya kutunuku Nishani ya Mapinduzi katika shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduziya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimtunuku Nishani ya Mapinduzi Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Ali Hassan Mwinyi,katika hafla kutunuku Nishani iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja, ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimtunuku Nishani ya Mapinduzi Viongozi wenye sifa Maalum kwa Dk. Salim Ahmed Salim, katika hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja, ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduziya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akimtunuku Nishani ya Mapinduzi Viongozi wenye sifa Maalum kwa Bw. Baraka Shamte, katika hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja, ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimtunuku Nishani ya Mapinduzi Viongozi Makundi na Wenye sifa Maalum kwa Bw. Col Soud Haji Khatib, katika hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja, ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduziya Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na kamati ya Nishani alipowasili katika uwanja wa Ikulu Mjini Unguja katika sherehe za kutunuku Nishani ya Mapinduzi kwa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Wastaafu, Viongozi walioasisi, kuenzi na kudumisha Mapinduzi, pamoja na Viongozi mbali mbali wenye sifa za Kipekee na wenye Sifa Maalum, katika shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisimama pamoja na Viongozi,Wananchi pamoja na Wakuu wa vikosi vya Ulinzi wakati wimbo wa Taifa Ukipigwa katika sherehe za kunuku Nishani ya Mapinduzi,katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)

No comments:

Post a Comment