TANGAZO


Saturday, January 11, 2014

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma awafanyisha awatahini viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali za Wilaya ya Kondoa kutathmini ufuatiliaji wao kiutendaji


Maofisa Tarafa wa tarafa nne (4) za Wilaya ya Kondoa, wakipitia maswali ya mtihani waliyopewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi (hayupo pichani), wenye lengo la kupima kiwango cha ufuatiliaji wa mambo na utendaji wa viongozi wa wilaya hiyo, mapema leo. (Picha zote na John Banda)
Wakuu wa Idara mbalimbali wilayani Kondoa wakijitahidi kujibu mtihani uliotolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (hayupo pichani), wenye lengo la kupima kiwango cha ufuatiliaji wa mambo na utendaji wa viongozi ngazi mbalimbali wilayani Kondoa kuanzia Watendaji wa Kata, Maofisa Tarafa, Wakuu wa Idara mpaka Mkuu wa wilaya hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi (kushoto), akisoma maelekezo ya mtihani aliowapa viongozi wa Wilaya na watendaji ngazi za juu wa Kondoa ili kupima kiwango cha ufuatiliaji wa mambo na utendaji wao wilayani humo mapema leo.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Omary Kwaangw' (kulia), akiumiza kichwa kutafuta majibu ya mtihani uliotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi (watatu kutoka kulia), ili kupima kiwango cha ufuatiliaji wa mambo na utendaji wa viongozi wa wilayani Kondoa. Zoezi hili litafanyika kwenye wilaya ya zote za Mkoa wa Dodoma. 
Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Kondoa, ambaye pia ni Ofisa Mteule Daraja la pili, Richard Mwita Marwa (kushoto), akisimamia mtihani uliotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa watendaji na viongozi wa Kondoa mapema leo.
Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Zabein Mhita akichangia hoja juu ya tathimini ya ufuatiliaji wa mambo na  utendaji wa viongozi na watendaji  wa Serikali wilayani Kondoa leo. Katikati ni Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Serikali za Mitaa, Dodoma Emanuel Kuboja na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi.

Na John Banda, Kondoa
WATENDAJI wa Serikali ngazi mbalimbali na viongozi wilayani Kondoa wakiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Omary Kwaangw' leo, wamefanya mtihani maalum wa kuandika uliokuwa unapima kiwango cha ufuatiliaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo na utendaji kwa ujumla.


Mtihani huo maalumu uliandaliwa na kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi na uliwahusisha viongozi Kondoa akiwamo Mkuu wa wilaya hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Wakuu wa Idara mbalimbali wilayani humo, Maofisa Tarafa wa tarafa nne (4) za wilaya hiyo na Watendaji wa Kata zote za wilaya  ya Kondoa.

Kwa mujibu wa Dk. Nchimbi ametumia mtihani huo kama njia mojawapo ya kufanya tathimini ya utendaji kazi na kiwango cha  ufuatiliaji wa masuala mbalimbali  ya msingi wilayani humo na kwamba makundi ya viongozi na watendaji waliohusika kwenye mtihani huo ndio haswa walengwa kwa kuwa wao ndio watendaji, wasimamizi, wafuatiliaji na kila kitu kinachotokea kuanzia
ngazi za msingi kwenye wilaya/maeneo yao ya uongozi ambapo amesema utaratibu huu wa mtihani  utafanyika kwenye wilaya zote za Mkoa wa Dodoma.


Wakati wa mtihani huo, Dk. Nchimbi alieleza kuwa sababu iliyomsukuma ni kufuatia mkoa hususani kwa wilaya zake kufanya vibaya kwenye baadhi ya sekta kama elimu, kilimo na uzalishaji wa chakula, ufugaji usio na manufaa tarajiwa, changamoto za afya, sekta ya maji, ardhi na maendeleo kwa ujumla wakati fursa zipo nyingi hivyo aliona kuna umuhimu wa kupima kama viongozi
na watendaji wanajihusisha na kufuatilia masuala mbalimbali ya maendeleo kuanzia ngazi za msingi.


Kwa mujibu wa maswali yaliyokuwepo kwenye mtihani huo uliotolewa na Mkuu wa Mkoa yalipima sana ufuatiliaji na utendaji kwenye sekta muhimu kama miundombinu, kilimo na uzalishaji wa chakula, maendeleo ya elimu, afya, maji, ufugaji na ardhi na utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa "big result now" (BRN)

Kwa upande wake Mbunge wa Kndoa Kaskazini Zabein Mhita akichangia juu ya utendaji wa watendaji amebainisha kuwa wapo watendaji wenye ufanisi, wapo ambao wana sifa na vigezo vizuri lakini utendaji wao hauendani na sifa zao nzuri,vilevile wapo waliozoea utaratibu wa utendaji wa "business as usual". Vilevile aliongeza kuwa wapo ambao hawana "commitment" wala morali
ya kazi, na pia wamekosa usiri.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Omary Kwaangw' amekiri kuwa changamoto kwa upande wa watendaji zipo na kutaja baadhi kama vile watendaji wenye elimu ndogo, na pia wapo waliokata tamaa na kazi kwa sababu mbalimbali ambapo alishauri ili kuendelea kuboresha ufanisi wa watendaji wao ni pamoja na kuwawezesha  watendaji wazikabili changamoto, kuwawezesha vitu kama vifaa vya usafiri, kuwapiga msasa wa mafunzo na motisha.

No comments:

Post a Comment