Raia wa Misri wameendelea na upigaji kura ya maamuzi kwa siku
ya pili ikiwa ni harakati za kupata katiba mpya tangu jeshi la nchi hiyo
kuuangusha utawala wa Rais wa zamani Mohammed Morsi.
Vituo vya upigaji kura vimekuwa vikifunguliwa saa tatu asubuhi huku vikosi vya ulinzi vikiimarishwa tangu siku ya Jumanne huku watu tisa wakiripotiwa kuuawa katika vurugu zilizotokea ambapo wengi wa waliouawa ni wafuasi wa Morsi.
Katiba mpya inayotarajiwa kupatikana nchini humo itachukua nafasi ya katiba ya zamani iliyopitishwa na Rais Morsi chini ya chama chake cha Muslim Brotherhood ambacho hivi karibuni kimetajwa kuwa ni kundi la kigaidi.
Wanajeshi wapatao 160,000 na polisi 200,000 wamesambazwa maeneo mbalimbali nchini humo kwa lengo la kudhibiti usalama.
No comments:
Post a Comment