Mjumbe wa ngazi ya juu katika Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa
jamii ya kimataifa kufanya juhudi zaidi kuisaidia Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Akiongea na BBC mjini Bangui, John Ging alisema kuwa nchi hiyo iko kwenye
mzozo mkubwa unaohitaji kutatuliwa.Kadhalika alisema kuwa wasiwasi mkubwa kwa sasa hivi ni kuwa hali huenda ikazorota zaidi.
Wiki jana,Umoja wa mataifa ulionya kuwa nchi hiyo inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kibinadamu kwa sababu watu wameanza kutoroka vita na kutafuta hifadhi katika kambi za muda.
Ameeleza kuwa kambi hizo hazina huduma muhimu na kuwa mazingira ni chafu.
Tayari kumekuwa na mlipuko wa Ugonjwa wa Surua katika uwanja wa ndege wa Bangui ambako watu 100,000 wamepata hifadhi .
Mjumbe huyo amesema kuwa idadi kubwa ya watu walioachwa bila makao,ni dalili ya kutosha kuwa mamilioni ya watu wamelazimika kutoroka makwao.
No comments:
Post a Comment