TANGAZO


Saturday, January 11, 2014

Mazishi ya marehemu Sultani Sikilo yafanyika Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam

Waombolezaji wakiuzika mwili wa aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) na Mweka hazina wa chama hicho, Sultani Sikilo katika Makaburi ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam leo. Sikilo alifariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baba wa marehemu, Sultani Sikilo, Saleh Sikilo, akiwa amemshikilia mtoto wa kwanza wa marehemu, Hossam Sultan, wakati wa mazishi yake kwenye makaburi hayo. Marehemu Sulu ameacha watoto wawili.
Baba wa marehemu, Sultani Sikilo, Saleh Sikilo, akiwa amemshikilia mjukuu wake, mtoto wa kwanza wa marehemu, Sullu, Hossam Sultani, wakati wa mazishi yake kwenye makaburi hayo. 
Waombolezaji wakiuzika mwili wa Sultani Sikilo katika Makaburi ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam leo. Sikilo alifariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi waliohudhuria mazishi hayo, wakiwa kwenye makaburi hayo wakati wa mazishi leo.
 Waombolezaji wakiuzika mwili wa Sikilo.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Jambo Concept, Benny Kisaka (kulia), akibadilishana mawazo na Alhaj Dk. Maneno Tamba (katikati) na mmoja wa ndugu wa familia ya marehemu Sikilo, Mbwana Chuma wakati wa mazishi hayo.
Waombolezaji wakilifukia kaburi lenye mwili wa marehemu Sultani Sikilo, wakati wa mazishi yake, Kibada leo.
Waombolezaji wakilifukia kaburi hilo, lenye mwili wa marehemu Sultani Sikilo, wakati wa mazishi yake, Kibada leo. 
 Waombolezaji wakilifuki kaburi lenye mwili huo.
 
Wahariri wa michezo wa Magazeyi ya Mwananchi, Ibrahim Bakari (kushoto), Frank Sanga (katikati) na Suleiman Jongo, wakiwa katika mazishi hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, inayochapisha magazeti ya Jambo Leo, Staa Spoti, Jarida la Jambo Brand na Dar Metro, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), Juma Pinto (kulia), akisalimiana na baadhi ya waandishi wa habari za michezo waliokuwepo katika mazishi hayo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto, akitaniana na baadhi ya waandishi wa habari za michezo waliokuwepo katika mazishi hayo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, inayochapisha magazeti ya Jambo Leo, Staa Spoti, Jarida la Jambo Brand na Dar Metro, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), Juma Pinto, akizungumza na baadhi ya waandishi wa habiri za michezo waliokuwepo katika mazishi hayo. 
Waombolezaji wakiuzika mwili wa marehemu Sulu Sikilo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiomba dua kwenye kaburi ulimozikwa mwili wa marehemu Sultani Sikilo mara baada ya kumalizikwa kwa shughuli za mazishi kwenye makaburi hayo ya Kibada leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiuombea dua mwili wa marehemu Sikilo, baada ya kuzikwa makaburini hapo leo.

No comments:

Post a Comment