TANGAZO


Thursday, January 2, 2014

Mauaji ya Karegeya kuchunguzwa

 

Ramani ya Rwanda
Polisi nchini Afrika Kusini wameanza kufanya uchunguzi kuhusiana na kifo cha mwanasiasa wa upinzani Patrick Karegeya, ambaye mwili wake, ulipatikana kwenye chumba cha hoteli mjini Johannesburg siku ya Jumatano.
Wanasema kuwa Bwana Karegeya huenda alinyongwa.

 
Shingo yake ilikuwa na uvimbe na polisi walipata taulo iliyokuwa na damu pamoja na kamba kwenye chumba ambapo maiti yake ilipatikana.
Bwana Karegeya, aliyekuwa mkuu wa zamani wa ujasusi na mshirika mkuu wa Rais Paul Kagame. Alitoroka Rwanda baada ya kutuhumiwa kwa kupanga njama ya kisiasa dhidi ya Rais Kagame mwaka 2006.
Aliishi kwa miaka mingi nchini Afrika Kusini ambako alifanikisha kuunda vuguvugu la upinzani.
Balozi wa Rwanda nchini Afrika Kusini Vincent Karega, alimtaja Karegeya kama adui lakini alikanusha madai kuwa serikali ya Kagame ndiyo imehusika na mauaji yake.
Bwana Karegeya amekuwa akiishi uhamishoni nchini Afrika Kusini kwa muda wa miaka sita iliyopita.
Karegeya alipokonywa cheo cha kanali baada ya kutofautiana na rais Paul Kagame.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, na chama cha upinzani cha Rwanda National Congress, RNC, inasema kuwa Karegeya alinyongwa ndani ya chumba chake.
Hata hivyo mamlaka nchini Afrika Kusini haijathibitisha madai hayo.

No comments:

Post a Comment