TANGAZO


Wednesday, January 15, 2014

JKT Makao Makuu kukipatia kompyuta 5 Kikosi cha Ruvu

Wapiganaji wa Kikosi cha Ruvu JKT (Wanaume), wakipita kwa ukakamavu mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Makao Makuu, Meja Jenerali Raphael Mhuga, wakati wa sherehe za amiaka 50 ya jeshi hilo, ambapo Kikosi cha Ruvu kimeadhimisha kwa shughuli mbalimbali, ikiwemo gwaride hilo lililofanyika kwenye Uwanja wa JKT Ruvu, Mlandizi Mkoa wa Pwani leo. (Picha zote na Omary Said)
Wapiganaji wa Kikosi cha Ruvu JKT (Wanawake), wakipita kwa ukakamavu mbele ya mgeni rasmi Muu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Makao Makuu, Meja Jenerali Raphael Mhuga, wakati wa sherehe za amiaka 50 ya jeshi hilo, ambapo Kikosi cha Ruvu kimeadhimisha kwa shughuli mbalimbali ikiwemo gwaride hilo, lililofanyika kwenye Uwanja wa JKT Ruvu, Mlandizi Mkoa wa Pwani leo.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Makao Makuu, Meja Jenerali Raphael Mhuga (katikati), akipokea kalenda ya mwaka 2014 kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Ruvu JKT, Luteni Kanali Charles Mbuge kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo na kikosi cha Ruvu. Sherehe hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa JKT Ruvu Mabatini. anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji mali la JKT (SUMA JKT), Brigedia Jenerali Mwanamakala Kilo.

Na Omary Said, Kibaha
JESHI la Kujenga Taifa (JKT) Makao Makuu limeahidi kukipatia kikosi cha Ruvu JKT kompyuta 5 na printa 2, ikiwa ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na uongozi wa kikosi hicho ambacho kinataraji kufungua huduma za Intanet, zinazohitaji kumi.

Kikosi hicho kilicho chini ya Mkuu wake Luteni Kanali Charles Mbuge kilichopo nje kidogo ya Mji wa Mlandizi Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, kipo katika mchakato wa kufungua huduma za intanet na saloon ya kisasa ambazo zinalenga kuwapatia huduma hizo maofisa wake na askari mbalimbali pia kuongeza mapato kwenye kikosi.

Ametoa kauli hiyo leo, ndani ya chumba hicho, alipopata  maelezo toka kwa Luteni Kanali Mbuge muda mfupi baada ya kukata utepe kwenye jengo hilo ambalo pia litakuwa na saloon ya kisasa, Meja Jenerali Raphael Mhuga alianza kwa kumpongeza Mbuge kwa juhudi anazozifanya kwa kushirikiana na maofisa wenzake katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Akiwa kwenye kambi hiyo, ambayo imesherehekea kuadhimisha kwa miaka 50 toka kuanzishwa kwa jeshi la Kujenga Taifa leo, limekuwa likitekeleza wajibu wake wa kuwalea vijana kwa viwango vya juu tangu kuanzishwa kwake.

"Kuundwa kwa jeshi hili Julai 10 mwaka 1963 lengo lake kuu ni kutoa fursa kwa wa-Tanzania hususani vijana kupata mafunzo mbalimbali ya ukakamavu, ujasiriamali na kuwa na moyo wa kuitumikia nchi yao," alisema Meja Jenerali Mhuga.

Ameongeza "Kama mnavyotambua mwaka jana tumepata bahati ya kuwapokea na kuwafundisha wabunge vijana ambapo lengo lake kuu ni kuwakumbushia baadhi ya maadili ya taifa kama nchi yao inavyoekwenda," alisema Meja Jenerali.

Aliongeza kuwa mwaka jana JKT imepata fursa ya kusherehekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwake Julai 10 mwaka 1963 ambapo katika kipindi hicho mambo mengi yamefanyika kupitia nyanja mbalimbali yote ikiwa ni kutimiza kusudio la kuanzishwa kwake.

Hakusita kuupongeza uongozi wa kikosi hicho kwa namna wanavyojituma katika kutekeleza majukumu yako ya kikazi sanjali na kutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana wanaopitia kwenye kikosi hicho.

Alisema kuwa kikosi cha Ruvu ndio kioo cha Jeshi la Kujenga Taifa, na kwamba wanapopata wageni kutoka nchi mbalimbali wanaotaka aidha kuanzisha jeshi, au kubadilisha muundo wa jeshi la kujenga taifa nchini mwao liwe chini ya wizara ya mambo ya ndani au chini ya vijana tunawalety huku ili kuona wanafanya nini.

"Kikosi cha Ruvu JKT kimepata mafanikio mengi tangu kilipoanzishwa, lakini kwenye kikosi hiki kwa uchache niombe niyataje haya yafuatayo, kimetimiza wajibu wake kwanza kuwapokea na kuwalea vijana, pili kimepokea vijana kwa mujibu wa sheria na wakujitolea wote wamekuwa wakipitia kikosi hiki," alisema Mkuu huyo wa JKT Makao Makuu.

Aidha ametoa pongezi kwa kuendeshwa miradi mbalimbali ikiwemo kilimo cha mpunga, bustani ya mbogamboga, ufugaji wa kuku, nyuki na ng'ombe na sasa kinataraji kuanzisha kilimo cha ufuta.

Akisoma taarifa yake mbele ya Meja Jenerali Mhuga, taarifa ya Luteni Kanali Mbuge imeeleza kwamba katika mikakati iliyopo ni pamoja na kuongeza ufugaji kuku kutoka 15,000 hadi kufikia 50,000, nyuki sanjali na kuanzisha shamba la ng'ombe wapatao 100.

"Mafanikio uliyoyaona kwa kiasi kikubwa yanatokana na miradi
kuendeshwa na viongozi wa vitengo usika kwa ushindani ambapo
wanaifanya vizuri wanazawadiwa na leo utatoa zawadi kwa viongozi waliofanya vizuri katika citengo vyao," ilieleza sehemu ya taarifa ya Luteni Kanali Mbuge.

No comments:

Post a Comment