Waziri wa ulinzi wa Israel Moshe Yaalon ameomba radhi kwa
matamshi yake yaliyochapishwa katika gazeti moja nchini humo, ya kumhujumu
waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry kuhusu anavyoshughulikia mzozo wa
Mashariki ya kati.
Hata hivyo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, bwana Yaalon amesema kuwa hakuwa na nia yoyote ya kumkosea heshima Kerry.
"Waziri wa ulinzi anaomba radhi ikiwa matamshi yake yamemuudhi bwana Kerry.’’
“Marekani na Israel zina lengo moja la kuendelea na mazungumzo na wapalestina,’’ ilisema taarifa hiyo.
"Tunamshukuru Kerry kwa juhudi zake kubwa kutafuta mwafaka wa Amani.’’
Ikulu ya White house imesema kwamba matamshi ya Israel hayafai kabisa ikizingatiwa kuwa Marekani inasaidia Israel kiuasalama.
No comments:
Post a Comment