Wasanii wa fensi ambao hujipaka mafuta machafu (mobile), wakiwa na mishale, wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi mbalimbali na wananchi waliohudhuria kuangalia fensi hiyo, iliyoshirikisha kazi za taasisi za Serikali na Binafsi, katika Barabara ya Kibandamaiti Mjini Unguja jana, ikiwa ni shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwapungia mkono wasanii wa asili na vikundi vya ngoma wakati Fensi katika barabara ya Kibandamaiti, Wilaya ya Mjini jana, katika shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Wengine waliokaa ni Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mwanamwema Shein.
Wasanii wakionesha namna ya tiba za asili kwa njia ya kupandisha mizuka ikiwemo ngoma za pungwa, wakati wa Fensi iliyopita katika barabara ya Kibandamaiti, Wilaya ya Mjini jana, katika shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Ngoma ya ndege ni miongoni mwa burudani za asili katika fensi zilizopita mbele ya mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, katika barabara ya Kibandamaiti, Mjini Unguja jana, ikiwa ni shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Baadhi ya wananchi wa Mji wa Unguja na vitongoji vyake, wakiangalia Fensi iliyopita katika Barabara ya Kibandamaiti, Mjini Unguja jana, ikiwa ni shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Ngoma ya Beni (Mbwa kachoka), ikipita mbele ya mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, katika barabara ya Kibandamaiti, Mjini Unguja jana, ikiwa ni shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Aina mabalimbali za miti ya asili, ikiwemo katika fensi, iliyopita katika Barabara ya Kibandamaiti, Mjini Unguja jana, ikiwa ni shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Kazi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi, zikioneshwa kwa wananchi mbalimbali waliofika kuangalia fensi katika barabara ya Kibandamaiti jana, ikiwa ni shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), akiwa ni mgeni rasmi.
No comments:
Post a Comment