TANGAZO


Wednesday, December 25, 2013

Watatu washikiliwa Morogoro wakiwa na maiti inayodaiwa kumeza kete za dawa za kulevya

 
Mwili  unaodaiwa kufarikid dunia baada ya kumeza  kete za dawa za kulevya ukiwa kwenye gari nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro leo. (Picha zote na Peter Kimath) 
 
Askari kanzu wakishusha mwili  unaodaiwa kufarikid dunia baada ya kumeza  kete za dawa za kulevya katika  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro leo.
 

 
 
Na Peter Kimath, Morogoro
 
WATU watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi  mkoani Morogoro kwa tuhuma za kusafirisha maiti inayosadikiwa kuwa na kete za dawa za kulevya tumboni na nyingine zikiwa zimehifadhiwa kwenye begi dogo kwenye buti la gari  aina ya spacial walilokuwa wakisafiria.

Chanzo cha habari kinasema kuwa  watuhumiwa hao, pamoja na marehemu walikuwa kwenye gari namba T887 BSW aina ya Spacial  wakitokea Tunduma mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam.

Ilidaiwa kuwa  baada ya kufika eneo la  Mikumi, wilayani
Kilosa, mkoani Morogoro, majira ya asubuhi leo, gari hilo lilisimamishwa na askari wa usalama barabarani na kukataa kusimamama, hivyo kuwapa mashaka askari hao.

Mara baada ya kuona gari hilo, limekataa kusimama ilibidi
walitilie shaka na kuamua kulifuatilia  huku gari hilo, likiwa na
mwendo kasi na baadaye askari kuamua kupiga risasi hewani na ndipo watuhumiwa hao wakasimama.

Baada ya kusimama, askari walianza kuhoji sababau ya wao kutosimama wakati wamewasimamisha na mmoja wa watuhumiwa hao kudai kuwa wanasafirisha maiti ya baba mkwe wake.

Aidha, baada ya kuhojiwa zaidi  na askari hao  na sababu za wao kukimbia alidai kuwa walikuwa hawana fedha za kusafirisha mwili huo, ndipo walikuwa wanahofia kukamtwa kutokan na kusafirisha kinyume na taratibu na sheria.

Hata hivyo, jopo la wanahabari lilishuhudia  askari wa upelelezi wa  Kituo kikuu cha Polisi mjini Morogoro, wakitoa kete saba za dawa za kulevya mbazo hazijafahamika aina yake, yakiwa katika  begi dogo, likiwa limehifadhiwa kwenye buti.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dr Litha
Lyamuya alisema mwili wa mwanaume  huyo ambaye umri wake haujafahamika umefanyiwa uchunguzi wa kidaktari na kukukutwa vitu  vinavyofanana na pipi.

Dk. Lyamuya alisema tayari taarifa zote wameziwasilisha polisi na kuwataka waandishi wa habari kwenda polisi ili kupata taarifa zaidi na kuweza kuwajulisha umma kilichotokea.
 

No comments:

Post a Comment