Viongozi kutoka Afrika mashariki wanatarajia kukutana nchini
Kenya kujadili kuhusu machafuko yanayokithiri nchini Sudani kusini, ambapo zaidi
ya Watu 1,000 wanaaminika kupoteza maisha.Mazungumzo hayo yanakuja siku moja
baada ya Rais wa Sudani kusini Salva Kiir kukutana na Mawaziri wakuu kutoka
nchini Kenya na Ethiopia.
Viongozi wa Jumuia ya Afrika Mashariki kutoka jumuia ya Igad watakutana jijini Nairobi kwa ajili ya kujadili maswala yaliyogusiwa katika mazungumzo yaliyofanyika siku ya Alhamisi kati ya Rais Kiir na Viongozi hao jijini Juba.
Wakati hayo yakijiri, Waziri wa Habari wa Sudani kusini Makuei Lueth ameliambia shirika la habari la AP kuwa mpaka sasa hakuna mawasiliano na Machar.
Sudani kusini imekuwa ikipigania kupata Serikali thabiti tangu kupata uhuru wao mwaka 2011, baada ya kujitenga.
No comments:
Post a Comment