Makamu Mwenyekiti UWT, Bi. Asha Bakari Makame akizunguza na wandishi wa Habari kuhusu miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo.
Makamu Mwenyekiti UWT, Bi. Asha Bakari Makame, akisisitiza jambo, alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari kuhusu miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Mjini Zanzibar leo.
Mwandishi wa habari wa Chuchu Fm Radio, Rahama Suleiman akitaka ufafanuzi wa kitu kwenye mkutano wa UWT, Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui Mjini Zanzibar leo. (Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Na
Ali Issa Maelezo-Zanzibar
UMOJA wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania
(UWT), umesema kuwa vikundi vingi vya ushirika vya akinamama vimesaidiwa
fedha nyingi za mikopo kujiendesha lakini inaonekana bado kuna baadhi ya
akinamama wanashindwa kuviendesha vikundi hivyo, kutokana na kutokuwa na dira
nzuri ya kuviendeleza vikundi hivyo.
Hayo yamesemwa leo, huko Ofisi kuu ya
Chama cha Mapinduzi Kisiwandui Mjini Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu wa UWT
Zanzibar Salama Aboud Talib wakati alipokuwa na mazungumzo na waandishi wa
Habari katika kuadhimisha sherehe za miaka 50 ya mapinduzi Zanzibar kwa Jumuiya
ya wanawake wa CCM Zanzibar.
Amesema umoja wa wanawake
Tanzania kupitia wake wa viongozi wa kuu wa Serikali na tasisi
nyengine wametoa pesa nyingi katika kusaidia vikundi vya kinamama
ili kujikwamua na umasini na kuviendeleza vikundi vyao kupata tija jambo ambalo
baadhi ya viongozi wa vikundi hivyo hushindwa kuviendeleza na
hatimae kutofikia malengo ya kuazishwa kwake.
Amesema hali hiyo si njema kwani
inarudisha nyuma juhudi za viongozi jambo ambalo lengo la chama cha Mapinduzi ni
kuijenga jamii ya wanawake kua na muelekeo mzuri kimaendeleo na kujinasua na
umasikini.
“Wake waviongozi wetu huwapa pesa
nyingi wana vikundi kuwasaidia wanawake lakini
vikundi hivyo hushindwa kuziendeleza pesa zile na baadae kikundi huwa kina
shindwa kujiendeshana pesa kupotea,” alisema Salama.
Aidha alifahamisha kuwa wanashindwa
kufahamu kupotea kwa pesa hizo kwani amesema kabla ya kutolewa peasa hizo
vikundi hupatiwa mafunzo kutoka kwa wataalamu ili waweze kuviendesha.
Bi.Salama alisema hali hiyo
haifurahishi hata kidogo kuona pesa zinapotea na vikundi kufa na italazimika kwa
wanavikundi kutafuta mbinu mbadala badala ya zile za kitalamu ili kuona vikundi
vina piga hatukubwa za kimaendeleo.
Nae
Makamo mwenyekiti UWT Bi. Asha Bakari Makame alisikitishwa sana na suala la
unyanyasaji kwa watoto na wanawake na kuishauri Serikali iangalie kwa umakini
suala hilo kwani inaonekana kuna mtandao mkubwa wa kuwadhalilisha watoto kwa
kuwanajisi hali ambayo ni hatari katika taifa hili la Zanzibar.
Amesema Serikali iangalie sheria zake
na kuzifanyia marekebisho kwani watoto wanaharibiwa vibaya na watuhumiwa
kushindwa kuingia hatiani jambo ambalo sisahihi kwa watoto kudhalilishwa kwa
kunajiwa na kutengwa na wazaziwao.
Makamo huyo alisifu juhudi za Jumuiya
hiyo inazochukua kwa kua karibu na wana nchi kupitia Serikali kuu kwa kufuata
ilani ya chama cha Mapinduzi.
Alisema hivi sasa wanawake wa
Zanzibar wamefaidika sana na Jumuiya hiyo kwa kupata frusa katika ngazi za
Sekikali na kuweza pia kupata elimu na ajira kwa idadi ya wanawake ambayo ni
wazi kuwa wanwake wa Zanibar wanathaminiwa sana na serikali yao.
Bi.Asha Bakari alizipongeza Serikali
zilizo pita,Viongozi wa Afroshirazi na hii ilioko madarakani kwa kuyaendeleza
Mapinduzi matukufu yalio mkomboa mwanamke kutoka katika utwala wakisultani na
1964 kua Taifa huru,lenye Umoja amani na
mshikamano.
No comments:
Post a Comment