Tabu Ley Rochereau, mwanamuziki maarufu na mwanzilishi wa
mtindo wa rumba wa soukous akijulikana kama"Mfalme wa Rumba la Congo" ambaye
alikuwa mmoja wa wanamuziki waliopendwa barani Afrika, amefariki Jumamosi katika
hospitali moja mjini Brussels, Ubelgiji.
Mwanamuziki Tabu Ley ambaye alikuja kushirikiana kimuziki na hata kimapenzi na mwanamuziki wa kike kutoka huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Mbilia Bel, alitikisa anga ya muziki wa rumba duniani, na hususan eneo la Afrika Mashariki na Kati.
Kwa mfano mwaka 1987 alifanya ziara nchini Tanzania, wakiwa na Mbilia Bel na kutembelea mikoa kadha, ikiwa ni kusherehekea miaka kumi ya kuzaliwa kwa chama tawala cha CCM, nchini Tanzania.
Miongoni mwa vibao vilivyompa umaarufu mkubwa Tabu Ley ni Muzina, Maze, C'est comme ca la vie, selikutu, Ibeba, Nadina na nyingine nyingi.
Wapenzi wa muziki wa rumba, watamkosa Tabu Ley, lakini wataendelea kuburudika na nyimbo zake ambazo alizitunga katika uhai wake, akiwa mwanamuziki.
No comments:
Post a Comment