TANGAZO


Thursday, December 26, 2013

Uturuki kufanya mabadiliko ya mawaziri

 


Receip Tayyip Erdogan

Waziri mkuu wa Uturuk Recep Tayyip Erdogan ametangaza kufanyika mabadiliko makubwa katika baraza la mawaziri nchini humo m kufuatia mawaziri wake watatu kujiuzuru kutokana na tuhuma za rushwa.
 
Katika mabadiliko hayo jumla ya Mawaziri 10 wapya watateuliwa ambao ni takribani nusu ya baraza zima la mawaziri

 
Uteuzi huo unatarajiwa kufanyika baada ya kuwa na mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Abdullah Gul ambaye amekubaliana na hatua hiyo
Mmoja wa mawaziri waliojiuzuru Erdogan Bayraktar aliyekuwa akiongoza wizara ya mazingira ametoa mtazamo wake tofauti kuhusiana na hatua hiyo akisistiza kwamba Waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan naye anapaswa kuachia madaraka
Polisi wanachunguza tuhumza za usafirishaji fedha kinyume cha sharia kwenda nchini Iran na madai ya kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika miradi ya ujenzi.

Aliyekuwa waziri wa mazingira Bayraktar, waziri wa uchumi Zafer Caglayan na waziri wa mabo ya ndani Muammer Guler walijiuzuru pale watoto watoto wao walipowekwa kizuizini ambapo hadi sasa viongozi hawa wote watatu wanapinga kutohusisha na tuhuma zozote.

Hata hivyo katika mji wa Istanbul waandamanaji walijitokeza mtaani wakipinga vitendo vya rushwa siku ya jumatano ambapo kulitokea machafuko Zaidi katika maandamano hayo.

Wachumabuzi wa masuala ya kisiasa wanasema huenda mvutano huo ni matokeo ya harakati za kutwaa madaraka kati ya serikali ya waziri mkuu Erdogan na kikundi kimoja cha kiislam chenye nguvu kinachoongozwa Fethullah Gulen ambaye nadhaniwa kuwa na idadi kubwa ya wafuasi nchini humo, ndani ya polisi na vyombo vya sheria

No comments:

Post a Comment