Jamii ya kimataifa inaendeleza juhudi za kujaribu kusitisha
mapigano yanayoendelea nchini Sudan Kusini.
Rais Salva Kirr amesema yuko tayari kwa mazungumzo ya amani, lakini hasimu wake mkuu, Riek Machar, anataka washirika wake waliokamatwa kuachiliwa huru kabla ya mazungumzo ya amani kuanza.
Mapigano yanaendelea katika kaskazini mwa nchi hiyo katika eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta, ambako wanajeshi wa serikali tayari wamekomboa miji kadhaa kutoka kwa wapiganaji wa upinzani.
Huku hayo yakijiri mapigano zaidi nchini Sudan Kusini yameripotiwa ambapo maelfu ya watu wanadaiwa kuuawa katika siku kumi za vita vya kikabila.
Msemaji wa jeshi la serikali amesema kuwa mapigano yanaendelea katika mji wa kazkazini wa Malakal ,licha ya wito wa umoja wa afrika kutaka vita hivyo kusitishwa siku ya krismasi.
Rais Salva Kiir pia alitoa wito wa mauaji kusitishwa akisema kuwa raia wasio na hatia wamekuwa wakiuawa.
Vita hivyo ni kati ya kabila la rais Kiir ,Dinka dhidi ya lile la Nuer la aliyekuwa makamu wake wa rais Riek Machar.
No comments:
Post a Comment