TANGAZO


Tuesday, December 24, 2013

TIGO YAZINDUA MASHINE ZA TIGO MATIC ZA KUTUMA NA KUPOKEA FEDHA MASAA 24


 Meneja Usuluhishi wa Malalamiko ya Wateja wa Kampuni ya Tigo, Henry Mboya (kulia), akizindua mashine mpya za Tigo Matic zinazowawezesha wateja wake kupata huduma za kutuma na kupokea fedha,kulipia bili za huduma mbalimbali, kuongeza salio na kupata laini mpya za simu. Anayeshuhudia uzinduzi huo uliofanyika Dar es Salaam leo, ni Mkuu wa Operesheni za Wateja wa Tigo, Zaeem Khan. (Picha zote na Kamanda Richard Mwaikenda)

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tigo yazindua mashine za ‘TigoMatic’ kutoa huduma masaa 24
Dar es Salaam, Desemba 24, 2013. Tigo Tanzania leo imetangaza uzinduzi wa mashine maalum zinazowawezesha wateja wake kupata huduma za kutuma na kupokea fedha, kulipia bili za huduma mbali mbali, kuongeza salio na kupata laini mpya za simu zinazofanya kazi masaa ishirini na nne kwa siku.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika tafrija ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez alisema kwamba mashine hizo zinazoitwa ‘TigoMatic’ zitawahudumia wateja aina wote, ikiwemo wateja wa malipo ya kabla na wateja wa malipo ya baadaye, zikifanya kazi masaa ishirini na nne kwa huduma zitolewazo na kampuni hiyo ya simu.
“Hakutakuwa na ulazima tena kwa wateja wetu kukaa kwenye foleni kwa ajili ya kupata huduma zetu kutoka kwenye matawi yetu na sehemu zetu mbali mbali za mauzo kwa sababu mashine hizi zitatoa msaada wa mteja kujihudumia mwenyewe,” alisema Bw. Gutierrez.
Alisema kwamba wateja wa Tigo hawatakuwa na ulazima wa kujisajili upya kwa ajili ya kutumia mashine hizo.
 
Akielezea jinsi mashine hizo zinavyofanya kazi, Bw. Gutierrez alisema kwamba Tigomatic ni mashine ambazo mteja anaweza akajihudumia yeye mwenyewe kama vile huduma za ATM ambapo mtu anaweza akafanya miamala tofauti tofauti bila kuhitaji kumtegemea mfanyakazi wa benki. 
Tigo ikiwa na wateja zaidi ya milioni 6 nchi nzima, Bw. Gutierrez amesema kwamba mashine hizo zitatolewa kwa awamu kuanzia Dar es Salaam siku ya leo (24 Desemba) kuelekea mikoa mengine mwakani. Mashine hizo zitawekwa katika sehemu za mikusanyiko mikubwa ya watu kwa mfano kwenye maduka makubwa, stendi za mabasi, barabarani, viwanja vya michezo na mahospitalini.
Mwisho.
Kwa ajili ya picha ya mashine ya ‘TigoMatic’ tafadhali wasiliana na muhusika hapo chini.

Kuhusu Tigo:
Tigo ni mtandao wa kwanza wa simu za mkononi nchini Tanzania. Ilianza shughuli mwaka 1994 na inapatikana katika mikoa thelathini (30) Tanzania bara na visiwani.
Lengo la Tigo ni kuwa mtandao unaoongoza kwa kutoa huduma bora na za ubunifu Tanzania kwa wateja wake wote ambazo zinaendana na mahitaji yao kuanzia huduma za sauti za bei nafuu, vifurushi vya intaneti vyenye kasi kubwa na huduma bora za fedha za simu za mkononi kupitia Tigo Pesa.
Tigo ni sehemu ya kampuni kubwa ya <
http://www.millicom.com/> Millicom
International Cellular S.A (MIC) ambayo ni ya unafuu wa huduma na inapatikana kirahisi  kwa zaidi ya wateja milioni 43 katika masoko 13 barani Afrika na Amerika ya Kusini.
"Tabasamu upo na Tigo"
Kwa taarifa zaidi tembelea
www.tigo.co.tz
Au wasiliana na:
John Wanyancha – Meneja Mawasiliano Tigo
Simu: +255 658 123 089
john.wanyancha@tigo.co.tz

No comments:

Post a Comment