Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dk. Servacius Likwelile akizungumza na waandishi wa habari9hawapo pichani) baada ya kusaini mikataba ya makubaliano na Serikali ya Ujerumani.Katikati ni Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi ya Dar es Salaam na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel.
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikataba iliyosainiwa kati ya Serikali yake na Serikali ya Tazania. Kushoto ni Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi ya Dar es Salaam Wolfgang Solzbacher.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dk. Servacius Likwelile akizungumza na waandishi wa habari9hawapo pichani) baada ya kusaini mikataba ya makubaliano na Serikali ya Ujerumani.Katikati ni Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi ya Dar es Salaam Wolfgang Solzbacher na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumzia jinsi mikataba hiyo itakavyonufaisha Hifadhi ya Serengeti huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dk. Servacius Likwelile Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi ya Dar es Salaam Wolfgang Solzbacher na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel, wakimsikiliza.
Picha ya pamoja kutoka kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel, atibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dk. Servacius Likwelile(mwenye suti ya kaki), Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi ya Dar es Salaam Wolfgang Solzbacher (mwenye tai nyekundu), Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Modestus Lilungulu na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi. (Picha zote na Hussein Makame, MAELEZO)
Hussein Makame, MAELEZO
SERIKALI ya
Tanzania na ile ya Shirikisho la Ujerumani zimesaini makubaliano ya msada wa
Fedha za Ulaya EURO Milioni 55.5 sawa na Shilingi Bilioni 121.89 za Kitanzania
kusaidia sekta ya Maji, Umeme na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Akizungumza
baada ya utiaji saini huo uliofanyika Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi
Dk. Servacius Likwelile alisema katika makubalianao ya kwanza Serikali ya
Ujerumani itatoa EURO Milioni 20.5 sawa na Shilingi Bilioni 45.059.
Alisema
fedha hizo zitatumika kusaidia Kuhifadhi wa Hifadhi ya Serengeti katika
Kuendeleza na Kutunza maliasili ya hifadhi hiyo, kuboresha miundombinu ya
kijamii na kujenga barabara katika wilaya za Loliondo na Srengeti.
“Mkataba wa makubaliano wa pili utawezesha
Serikali ya Ujerumani kutoa mchango wa EURO Miloni 20 sawa na Shilingi Bilioni 43.96 kusaidia
kusambaza umeme Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania “ alisema Dk. Likwelile.
Alisema
msaada huo utasaidia kuunganisha wananchi wa vijijini 32,500 katika maeneo hayo
kupata umeme na kuunganisha Gridi ya Taifa hadi kwenye Mtambo wa Kuzalisha
Umeme wa maji wa Rusumo na kuuza umeme nchini Rwanda na Burundi.
Dk.
Likwelile aliongeza kuwa mkataba wa makubaliano wa tatu utaiwezesha Serikali ya
Ujerumani kutoa msaada wa EURO Milioni 15 sawa na Shilingi Bilioni 32.97
kusaidia Sekta ya Maji kupitia Programu ya Maendeleo awamu ya pili.
Alifafanua
kuwa kupitia programu hiyo msaada huo utafabikisha utekelezaji wa Usimamizi wa
Rasilimali ya Maji, Usambazaji wa maji Vijijini na Mijini na Kuimarisha Taasisi
na Kujengea Uwezo Sekta ya Maji.
Aliihakikishia
Serikali ya Ujerumani kuwa fedha hizo zitatumika vizuri na kuwanufaisha
wananchi wa maeneo husika na aliwaomba wanachi husika wathamini msaada huo kwa
kutunze miradi ya maendeleo katika maeneo hayo.
Balozi wa
Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel msaada huo unathibitisha kuwa Serikali
yake imedhamiria kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo ili kuchangia kuboresha
ustawi na utajiri wa wananchi wa Tanzania.
Naye Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Modestus Lilungulu alisema msaada huo utasaidia
kutekeleza Mkakati wa Matokeo Makubwa Sasa ambao lengo lake ni kufikisha huduma
ya maji vijijini kwa asilimia 74 na mijini asilimia 90 ifikapo mwaka 2015.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi
alisema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati muwafaka kutokana na changamoto ya
ongezeko la idaidi ya watu lililosababisha kuongezeka kwa huduma kwa binadamu
kuongezeka.
Kwa zaidi ya
miongo mitano iliyopita Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Ujerumani
umefanikisha misaada yenye thamani ya Fedha za Ulaya EURO Bilioni 2.03 huku
Serikali ya Ujerumani ikisaidia sekta za Umeme, maji, mazingira na Afya.
No comments:
Post a Comment