TANGAZO


Monday, December 16, 2013

Huduma ya M-Pesa yazinduliwa Uchumi Supermarket

*Vodacom yazindua pia duka ndani ya Supermarket hiyo, kupunguza usumbufu kwa wateja

Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom, Salum Mwalimu, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati kampuni hiyo na Uchumi Supermarket, walipozindua ushirikiano wa biashara ya manunuzi kwa kutumia huduma ya M-Pesa na pia Vodacom kuzindua duka lake kwenye Supermarket iliyopo kwenye jingo la Quality Plaza jijini. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom, Salum Mwalimu, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati kampuni hiyo na Uchumi Supermarket, walipozindua ushirikiano wa biashara ya manunuzi kwa kutumia huduma ya M-Pesa na pia Vodacom kuzindua duka lake kwenye Supermarket iliyopo kwenye jingo la Quality Plaza jijini.
Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Tanzania, Chris Linana (kulia) na Ofisa Mkuu, Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh, wakikata utepe ili kuzindua duka la Vodacom ndani ya Supermarket hiyo, litalotoa huduma mbalimbali kwa wateja wa kampuni hiyo. Pia Vodacom kwa kushirikiana na Uchumi Supermarket, wamezindua huduma ya manunuzi kupitia huduma ya M-Pesa kwenye Superket hiyo, iliyopo Qulity Centre, Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam leo.  
Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Tanzania, Chris Linana, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo.
Ofisa Mkuu, Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi huo. Kushoto ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom, Salum Mwalimu.
Ofisa Mkuu, Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh, akifanya manunuzi Uchumi Supermarket wakati wa uzinduzi wa huduma ya M-Pesa na duka la Vodacom kwenye Supermarket hiyo leo. Wanaoshuhudia ni Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Tanzania, Chris Linana (kushoto) na kulia ni Mkuu wa Idara ya Maduka ya Vodacom, Upendo Richard. 
Ofisa Mkuu, Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh, akifanya manunuzi Uchumi Supermarket wakati wa uzinduzi wa huduma ya M-Pesa na duka la Vodacom kwenye Supermarket hiyo leo. Wanaoshuhudia ni Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Tanzania, Chris Linana (wa pili kushoto), Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom, Salum Mwalimu (kushoto) na kulia ni Mkuu wa Idara ya Maduka ya Vodacom, Upendo Richard.
Ofisa Mkuu, Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh, akikabidhiwa risiti yake na mhudumu wa Uchumi Supermarket baada ya kununua bidhaa kupitia huduma ya M-Pesa Wanaoshuhudia ni Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Tanzania, Chris Linana (katikati) na kushoto ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom, Salum Mwalimu.
Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Tanzania, Chris Linana (kushoto), akimuonesha jinsi ununuzi wa M-Pesa, unavyofanyika kwenye kompyuta, Ofisa Mkuu, Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh, mara baada ya kuzindua huduma ya manunuzi pamoja na duka la Vodacom kwenye duka hilo, lililopo Qulity Centre, Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Maduka ya Vodacom, Upendo Richard na kushoto ni muuzaji wa Uchumi Super Market, Emmanuel Lyimo.

KATIKA muendelezo wa mapinduzi ya kuyaleta maisha kiganjani, sasa wateja wanaofika kupata huduma kwenye SuperMarkert ya Uchumi lililopo katika jengo la Quality Center jijini Dar es salaama wanauwezo wa kulipia huduma zao kwa njia ya M-pesa.
Aidha, Vodacom pia imefungua duka la huduma kwa wateja wake ndani ya Supermarket hiyo ikiwa ni ubunifu wa aina yake hapa nchini na hivyo kuwapa nafasi ya kipekee wateja wa Vodacom kumaliza mahitaji yao yote kwa nwakati mmoja
“Tunazidi kuongoza katika ubunifu hili ni jambo tunalolipa kipaumbele kw alengo la kuhakikisha tunatoa nafasi kwa wateja wetu kufaidi matumizi ya teknolojia na kubadili maisha yao, hakuna shaka kila tunachokifanya kinawatimiza matarijio yao kwetu.”Alisema Ofisa Mkuu wa Mauzo na Mahusiano wa Vodacom
Kila mmoja Wakati huu w amsimu wa siku kuu angependa kuona anatumia muda mfupi na kwa urahisi zaidi kupata huduma, hatua moja muhimu ni kuwawezesha kuwa na njia rahisi na nyepesi zaidi ya kukamilisha mahitaji yao na hivyo ndivyo tunavyofanya leo kwa kuwatanagzi wateja wetu kutumia M-pesa wanapofika Uchumi SuperMarket.”Aliongeza
 Kwa sasa M-pesa inawaunganisha wateja wetu na biashara zaidi ya 300 katika Nyanja mbalimbali ikiwemo kulipia tiketi za ndege ving’amuzi,LUKU, maji, kutoa na kuweka fedha katika akaunti za benki zaidi ya 20 na hivyo kuongoza soko miongoni mwa huduma za fedha kwa njia ya simu.. Kwa upande wake Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Tanzania, Chriss Lenana amebainisha kuwa ni jambo la furaha na kujivunia kuzinduliwa kwa ubia huo kati ya kampuni yake na Vodaco na hivyo kuwawezesha wateja wake kutumia simu zao kwa ajili ya malipo ya manunuzi.
 “Kufunguliwa kwa duka la Vodacom hapa kwetu kutasaidia sana wateja wetu si tu kuweza kupata huduma za M – PESA bali pia huduma nyingine za kimawasiliano na hatimaye kuepukana na matatizo ya kimawasiliano yanayowakabili. Tunapokea idadi kubwa ya wateja kila kukicha na kwa kufunguliwa kwa duka hili Vodacom wamefanya suala la msingi ambapo awali iliwalazimu wateja kusafiri mpaka makao makuu kufuata huduma hizo kitu ambacho ni usumbufu na kiusalama ni changamoto.” Alisema  Lenana
“Huduma hii ya malipo kwa njia ya M-pesa tutaisamabza kwenye maduka yetu yote ambayoyapo kwenye mipango yetu ya mwaka 2014/2015, ni wazi tumewaptia wateja wetu kitu kizuri na tunawaomba watumie njia hii ya malipo kwa kujiamini kwani mteja hupatiwa pia stakabadhi ya mununizi”Aliongeza
Duka hilo ni moja kati ya maduka 200 ya Vodacom ambayo yapo mbioni kufunguliwa nchi nzima na pia ni muendelezo wa uboreshwaji wa huduma ya M – PESA na huduma nyinginezo za kampuni hiyo nchi nzima.

No comments:

Post a Comment