Baadhi ya wananchi waliofika katika hafla ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani, wakisoma vjarida vilivyotolewa katika
maadhimisho hayo, yaliyofanyika Paje, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja, mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.
Wananchi wa vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Kusini Unguja, wakiwa katika hafla ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani,
ambapo kwa mwaka huu, Kijiji cha Paje, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja, yamefanyika maadhimisho hayo, na mgeni
rasmi akiwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika Kijiji cha Paje, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja, mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.
Vijana wa Zapha+ ni watu wanaoishi na Virusi vinavyosababisha Ukumwi, wakifanya igizo, mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani), pamoja na wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika Kijiji cha Paje,Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja leo.
Bibi Fauzia Ismail Aboud, kutoka Shirika la PSI
Tanzania,akisoma risala wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi
Duniani yaliyofanyika Kijiji cha Paje,Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini
Unguja, akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma
Abdulhabib Fereji,alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili
kushoto),kuzungumza na wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya
ukimwi Duniani yaliyoafnyika leo katika Kijiji cha Paje,Wilaya ya
Kusini,Mkoa wa Kusini Unguja,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati), alipokuwa akizungumza na wananchi katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani, yaliyofanyika
leo, katika Kijiji cha Paje, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini
Unguja. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dk. Idrisa Muslim Hija.
Wasoma Utenzi kutoka Makunduchi, Asia Bukheti (kulia) na Amina Haji Simai, wakitoa burudani hiyo, leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya ukimwi duniani, yaliyoafanyika leo, katika Kijiji cha Paje, Wilayay a Kusini,Mkoa wa Kusini Unguja,mbele ya mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia), akiiangalia picha yake wakati alipokuwa Meneja wa Mradi wa Kitengo cha Ukimwi kutoka Nov 1997- Julai, mwaka 1998, wakati wa maonesho katika banda la kitengo cha Ukimwi cha Wizara ya Afya, wakati wa maadhimisho ya Siku ya ukimwi Duniani, yaliyofanyika leo, katika Kijiji cha Paje, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja. Kulia ni Dk. Ahmed Khatib wa Kitengo cha Ukimwi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia), akiangalia vifaa mbalimbali
wakati alipotembelea banda la kitengo cha Ukimwi cha Wizara ya
Afya, wakati wa maadhimisho ya Siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika leo katika Kijiji cha Paje, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja. Kulia ni Dk. Mohamed Khatib, Meneja wa Kitengo cha Ukimwi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dk. Ali Mohamed Shein (kulia), akipatiwa maelezo kutoka kwa Dk. Farhat Khalid wa kitengo cha Ukimwi, wakati alipotembelea maonesho katika banda la kitengo cha Ukimwi la Wizara ya Afya, wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani, yaliyofanyika leo, katika Kijiji cha Paje, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdulhabib Fereji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na jumuiya ya Zayedesa, wakati alipotembelea mabanda mbalimbali ya maonesho yanayojishughulisha na kutoa elimu ya Ukimwi wakati
wa Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani, Kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika leo, katika Kijiji cha Paje, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja
WANANCHI
wa Zanzibar wametahadharishwa kutojenga dhana kuwa asilimia 1.0 ya watu
wanaoishi na virusi vya ugonjwa wa UKIMWI Zanzibar ni ndogo ikilinganishwa na
nchi nyingine zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako maambukizi katika nchi
hizo kwa mujibu wa tafiti za mwaka 2011 yalikuwa ni asilimia 4.9.
Tahadhari
hiyo imetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali
Mohamed Shein wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani
yaliyofanyika kitaifa Zanzibar katika kijiji cha Paje Mkoa wa Kaskazini
Unguja.
Kwa
hiyo ametoa wito kwa wananchi wa Zanzibar kushirikiana na kuunga mkono juhudi
mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali na taasisi za ndani na nje ya nchi kuzuia
maambukizi mapya ya virusi vya ugonjwa huo.
Akitoa
takwimu za hivi karibuni kuhusu maambukizi ya ugonjwa huo Zanzibar Dk. Shein
alinukuu matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Ugonjwa wa UKIMWI na Malaria wa
mwaka 2012 ambayo yalionyesha kuwa maambukizi ya ugonjwa huo Zanzibar
yameongezeka kwa asilimia 0.4 kutoka asilimia 0.6 mwaka 2008 hadi asilimia 1.0
mwaka 2012.
Alifafanua
kuwa kutokana na takwimu hizo na kwa sababu matokeo ya Sensa ya Watu na Maakazi
ya mwaka 2012 yanaonyesha kuwa Zanzibar ina wakazi 1.3 milioni kwa hiyo watu
30,000 ambao ni asilimia moja ya idadi hiyo wanaishi na virusi vya ugonjwa huo
Zanzibar.
Kwa
hiyo alisisitiza kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kushiriki katika kupiga vita
unyanyapaa na ubaguzi wa aina yeyote ile dhidi ya waathirika wa ugonjwa huo
ikiwa ni njia bora ya kuwatia moyo waathirika hao ili waweze kufaidika na
jitihada mbalimbali zinazosaidia kupunguza nguvu za maradhi hayo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliwahakikishia
mamia ya wananchi na washirika katika mapambano dhidi ya ugonjwa
huo kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea na jitihada zake za
kupambana na ugonjwa huo kupitia programu mbalimbali za Afya pamoja na mipango
mingine ya maendeleo ikiwemo MKUZAII.
Sambamba
na mipango hiyo, alieleza kuwa nia ya Serikali vile vile ni kuendelea kuongeza
bajeti ya fedha katika miradi ya kupambana na ugonjwa wa UKIMWI kadri uwezo wa
kifedha unavyoruhusu.
Aliwataka
wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo na wale wanaofuatilia kupitia vyombo vya
habari kuzingatia ujumbe wa mwaka huu wa maadhimisho hayo ambao ni kuondoa
‘zero’ tatu ifikapo mwaka 2015. Ziro hizo tatu hizo ni kusiwepo maambukizi
mapya, kusiwepo unyanyapaa, na kusiwepo vifo vitokanavyo ya UKIMWI.
Dk.
Shein aliwakumbusha wananchi kuwa katika jitihada za kupamba dhidi ya maambukizi
mapya kuzingatia maadili mema na kufungamana na mafundisho ya dini pamoja
na utamaduni wa nchi.
Alitumia
fursa hiyo kuzipongeza na kuzishukuru taasisi zisizo za kiserikali nchini kwa
jinsi zinavyoshiriki katika vita dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI pamoja na huduma
zinazozitoa kwa waathirika wa ugonjwa huo.
Awali
akizungumza katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI
Zanzibar Profesa Saleh Mohamed Idrissa alieleza kuwa katika kipindi cha mwaka
mmoja uliopita mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kupanua shughuli za huduma
na tiba kwa mujibu wa Mwongozo wa WHO kwa wenye virusi vya kiwango cha CD4 350
badala ya kile cha zamani cha CD4 200.
Aliongeza
kuwa hadi Disemba mwaka jana asilimia 55 ya watu wanaoishi na VVU kwa kutumia
kigezo cha CD4 chini ya 200 walikuwa wakipatiwa dawa wakati hadi Juni 2013 idadi
ilifikia asilimia 63 kwa kutumia kiwango cha CD4 350.
Profesa
Idrisa alibainisha kuwa huduma za kupima kwa hiari zimeongezeka kutoka watu 86
mwaka 1986 hadi kufikia watu 87,326 mwaka 2012 ambapo kwa upande wa upimaji wa
VVU kwa kina mama wajawazito kwa kipindi cha Januari hadi Septemba 2013 pekee
jumla ya mama wajawazito 38,555 walipimwa katika vituo 151.
Katika
risala yao Jumuiya ya Watu Wanaoishi na VVU/UKIMWI Zanzibar (ZAPHA+) pamoja na
kuishukuru Serikali na taasisi nyingine kusaidia watu wanaoishi na VVU lakini
walieleza wasiwasi wao kufikia malengo ya ujumbe wa maadhimisho ya mwaka
huu.
Walieleza
kuwa vifo vinavyotokana na UKIMWI havitaweza kuepukika endapo jamii haitachukua
jitihada za makusudi kuondoa unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu wenye VVU
hususan watoto wanaoishi na virusi vya ugonjwa huo ambao wanahitaji matunzo
muhimu kama chakula, matibabu na elimu.
Risala
hiyo iliyosomwa na Saade Said Saadun ilieleza kuwa unyanyapaa na ubaguzi kwa
watu wanaoishi na VVU ndio adui mkubwa wa mapambano dhidi ya UKIMWI kwa kuwa
waathirika hawataweza kujitokeza kupata tiba wala huduma nyinginezo zitolewazo
na jamii.
Maadhimisho
hayo yalihudhuria pia na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd pamoja na
viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu na washirika katika
mapambano dhidi ya UKIMWI.
No comments:
Post a Comment