TANGAZO


Sunday, December 1, 2013

Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa Geneva, Balozi Modest Mero awasilisha hati za utambulisho kwa Roberto Azevedo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara la Kimataifa Duniani yaani World Trade Organisation (WTO) mjini Geneva, Uswisi

 Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania  katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Roberto Azevedo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara ya Kimataifa  Duniani yaani World Trade Organisation(WTO) mjini Geneva, Uswisi.
  Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania  katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva katika mazungumzo.
Picha ya pamoja Balozi Mero, Mama Mero na Bw. Azevedo.
-----
Mheshimiwa Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania  katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva amewasilisha hati za utambulisho kwa Bw. Roberto Azevedo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara ya Kimataifa  Duniani yaani World Trade Organisation(WTO) mjini Geneva, Uswisi.
 Katika mazungumzo,  Mkurugenzi Mkuu amemfahamisha Mh. Balozi  kuwa Shirika la Biashara Duniani liko katika hatua za mwisho kukamilisha  majadiliano ya mikataba ya  Biashara ya Kimataifa katika maeneo matatu kwa pamoja  ikiwa ni masuala ya  Kilimo,  Maendeleo na  Uwezeshaji Biashara.
Aidha,  Mkurungenzi Mkuu alielezea  mahusiano mazuri aliyonayo na nchi yetu kwa kipindi  kifupi akiwa kama Mkurugenzi Mkuu,  na  kuwa aliliona hilo wakati wa kampeini yake alipokuja nchini kuomba kura yetu. Ni kwa mantiki hiyo na imani aliyo nayo kwa Tanzania, Mkurugenzi huyo ameomba Tanzania itumie ushawishi wake ili kufanikisha mkutano wa Mawaziri wa Biashara utakaofanyika mjini Bali Indonesia kuanzia tarehe 3-6 December 2013, ili kupitisha mikataba ya Biashara katika maeneo  matatu yaliyotajwa hapa juu.

No comments:

Post a Comment