Marekani imesema kuwa inasikitishwa na machafuko yanayoendelea
nchini Jamuhuri ya afrika ya kati, huku Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John
Kerry akizitaka mamlaka kufanya uchaguzi haraka iwezekanavyo.
Watu kadhaa wameuawa wakiwemo walinda amani kutoka nchini Chad kutokana na
machafuko yanayoendelea nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati maafisa nchini humo
wameeleza.Shirika la misaada la msalaba mwekundu limesema Watu wengine takriban 40 wameuawa tangu siku ya jumatano.
Umoja wa Afrika umepeleka wanajeshi wake 4,000 nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati. Ufaransa ambalo ni koloni la zamani la nchi hiyo likiwa na Wanajeshi wake 1,600 kwa ajili ya kuimarisha hali ya usalama.
Wanamgambo kutoka jamii ya kikristo na kiislamu wamekuwa wakishambuliana tangu Mitchel Djotodia alipokuwa Kiongozi wa Taifa hilo baada ya kumuondoa madarakani Francois Bozize anayetoka jamii ya kikristo.
Wakristo wengi wamekuwa wakiishutumu Serikali ya Chad kuwa na uhusiano na Waasi wa Seleka waliomuweka madarakani Djotodia, huku waislamu nao wakishutumu majeshi ya ufaransa kuwa yamekuwa yakishirikiana na wanamgambo wa kikristo
No comments:
Post a Comment