TANGAZO


Saturday, December 14, 2013

Malkia Maxima wa Uholanzi atembelea miradi ya Kilimo, Dodoma

 
Malkia Maxima wa Uholanzi akiwa ameongozana na Mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi muda mfupi baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma kufanya ziara kutembelea miradi ya kilimo, inayofadhiliwa na Shirika la Chakula Duniani (WFP), Manispaa ya Dodoma, vilevile kukutana na wakulima wadogo wadogo wa Wilaya za Dodoma leo hii. (Picha zote na John Banda)
Malkia Maxima wa Uholanzi akisalimiana na kiongozi wa kundi la ngoma za asili la Hiyari ya Moyo, Musa Mwinamila muda mfupi baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo, maalumu kwa ajili ya kufanya ziara ya kutembelea miradi ya kilimo inayofadhiliwa na WFP, Manispaa ya Dodoma.
Malkia Maxima wa Uholanzi akivishwa mavazi ya asili ya Wagogo, kaniki na kibuyu na mmoja wa wakulima wadogowadogo wa zabibu wa Kijiji cha Gawae, Manispaa ya Dodoma wakati Malkia huyo, alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya kilimo inayofadhiliwa na WFP, Manispaa ya Dodoma leo hii.

No comments:

Post a Comment