TANGAZO


Sunday, December 1, 2013

Makamu Rais, Dk. Gharib Bilal awa mgeni rasmi maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwai, chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Angela Ramadhan, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, yaliyofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa
Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dk. Fatma Mrisho. (Picha na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifurahi na mtoto Samir Isagetee (miezi 7), akiwa na mama yake, Lilian Amani, wakati alipotembelea banda la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi(NACOPHA), katika
Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, zilizofanyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Mtoto huyo ni mmoja kati ya watoto waliozaliwa na wazazi wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi na yeye kuzaliwa salama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda katika maadhimisho hayo. 
Baadhi ya wanafunzi wakipita na mabango yenye ujumbe mbalimbali mbele ya jukwaa kuu, wakati Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal, alipokuwa akipokea maandamano, kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanafunzi wakipita na mabango yenye ujumbe mbalimbali mbele ya jukwaa kuu, wakati Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal, alipokuwa akipokea maandamano, kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Mpango Mkakati wa 3 wa Kitaifa wa Kudhibiti Ukimwi (NMSF3), wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantum Mahiza (wa pili kulia) na Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dk. Fatma Mrisho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi moja kati ya vitabu vya Mkakati wa 3 wa Kitaifa wa Kudhibiti Ukimwi (NMSF3), Sheikh  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, baada ya kuzindua mpango mkakati huo, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi, Mashine za CD4 kwa ajili ya Kanda za Juu Kusini, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wakati wa maadhimisho hayo.

No comments:

Post a Comment