Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani jana, 24/12/2013. Bwana Ban Ki Moon alimwalika Rais Kikwete ambapo viongozi hao wawili, walijadili masuala mbalimbali ya Kimataifa hususan masuala ya amani na ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika kudumisha amani sehemu mbalimbali Afrika na katika nchi nyingine duniani. Tanzania ina majeshi ya kulinda amani katika nchi kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Darfur nchini Sudan na Lebanon.
Rais Kikwete yupo jijini New York nchini Marekani ambapo anaendelea vyema na ukaguzi wa kawaida wa afya yake.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki Moon jana.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon (kulia), akiagana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya mazungumzo yao kwenye Ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani jana, 24/12/2013. (Picha zote na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment