Bunge la Somalia limeanza kujadili hoja ya kutokuwa na imani na
Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdi Farah Shirdon ambaye amekuwa haelewani na rais wa
nchi hiyo Hassan Sheikh Mahamud.
Wafuasi wa rais Hassan wanasema Waziri Mkuu huyo ameshindwa kutekeleza majukumu yake na uongozi wake umekuwa hauna mafanikio.
Mwandishi wa habari wa BBC aliyepo Somalia anasema mgawanyiko katika serikali ya Somalia iliyoundwa mwaka jana, unatishia juhudi za kuimarisha utulivu nchini humo baada ya nchi hiyo kuathirika na mgogoro kwa takrabani miongo miwili.
No comments:
Post a Comment