TANGAZO


Tuesday, December 17, 2013

Daktari mwokozi afia gerezani Syria

 


Daktari Khan alikwenda Syria kutoa msaada wa kimatibabu

Familia ya daktari mmoja wa Uingereza ambaye inasemekana amezuiliwa nchini Syria,inasema kuwa amefariki.
 
Daktari Abbas Khan mwenye umri wa miaka 32 mtaalamu wa upasuaji kutoka London, alienda Syria kuwasaidia waathiriwa wa mgogoro wa kisiasa unatokota nchini humo.

 
Alizuiliwa Kaskazini mwa Syria mwezi Novemba 2012.
Khan alienda nchini Syria kuwasaidia waathiriwa na vita vya wenyewe kwa wenyewer vinavyoendelea nchini humo.

Alikuwa amekaa mjini Aleppo kwa masaa 48 pekee alipokamatwa na kutoka hapo amekuwa akizuiliwa katika chumba chake pekee kwa mwaka mmoja uliopita huku akiteswa kulingana na barua alizokuwa anatuma nyumbani Uingereza.

Kifo chake bila shaka ni pigio kubwa kwa familia yake ambayo ilikuwa inamsubiri arejee nyumbani.

Lakini wamefahamishwa na maafisa wakuu nchini Syria kuwa alikuwa anarejea nyumbani wakati atakapoachiliwa katika muda wa siku chache zijazo.
Kisha afisaa mmoja akawapigia simu kuwaarifu kuwa Khan alipatikana akiwa amejitoa uhai ndani ya chumba chake
Lakini familia ya Khan inasema kuwa hawaamini kauli ya maafisa wa Syria.
Hata hivyo inaarifiwa kuwa kifo cha daktari Khan huenda kilitokea kutokana na mvutano kati ya serikali ya Rais wa Syria na maafisa wake wa usalama . Ni Rais Assad pekee ambaye angeweza kuamuru kuachiliwa kwa daktari huyo ,hatua ambayo ingekuwa ishara njema kwa mkutano wa amani ambao Uingereza inasaidia kuandaa kwa niaba ya Syria.

Baadhi ya maafisa katika serikali ya Assad serikalini hawataki mazungumzo hayo yafanikiwe.

No comments:

Post a Comment