TANGAZO


Tuesday, December 17, 2013

Bbc swahili: Habari kwa njia ya kisasa

 


Sura mpya ya habari za bbcswahili.com kwenye simu yako ya mkononi


17 Disemba 2013. Watumiaji wa Idhaa ya Kiswahili kupitia simu za mkononi sasa wataanza kupata huduma bora zaidi za kisasa (digitali) baada ya Idhaa hiyo kuanzisha mbinu shirikishi kwa watumiaji wake.

 
Sasa watumiaji wenye simu ya aina yeyote kuanzia simu za kawaida hadi za kisasa (smartphones) wataweza kuunganishwa moja kwa moja kwenye mfumo uliobuniwa kuendana na aina ya simu wanazotumia kupata habari.
Karibu 90% mawasiliano ya mtandao wa Idhaa ya Kiswahlili kwenye internet yanafanyika kupitia simu za mkononi.

Mhariri wa Idhaa hiyo, Ali Saleh, anasema: “Kutokana na kuwa wengi wa wasikilizaji wetu kwenye mtandao wanatupata kupitia simu za mkononi, tunafurahi kuwa wa kwanza miongoni mwa watoa habari kupitia mtandao kwa lugha ya Kiswahili, kwa njia ya simu, kuanzisha teknolojia hii shirikishi ili waweze kufurahia huduma ya mtandao wa bbcswahili.com kwa ubora wa hali ya juu, bila kujali aina ya simu wanazotumia.”

Kubuniwa na kutumika kwa Teknolojia hii Shirikishi kwenye mtandao wabbcswahili.comni sehemu ya uwajibikaji wa Shirika la BBC kuwashirikisha zaidi wasikilizaji wake kupitia simu za mkononi. Idhaa ya BBC Duniani (BBC World Service) inafanya jitihada kupanua teknolojia hii iliyosanifiwa kuwa Shirikishi ifikie kiwango cha kutumika kwenye tabiti na komputa za mezani.

No comments:

Post a Comment