Wanachama wa Chama cha African National Congress (ANC) wametoa
heshima za mwisho kwenye mwili wa Hayati Nelson Mandela kabla ya kuzikwa hapo
kesho.
Rais Jacob Zuma na viongozi wengine wa ANC walihudhuria tukio hilo
iliyopambwa na sala za viongozi wa mbali mbali wa dini pamoja na muziki.Karibu watu wanachama 1000 wa ANC ambacho kiliwahi kuongozwa na Hayati Mandela wamehudhuria zoezi hilo la kutoa heshima za mwisho kwenye ngome ya jeshi la anga Waterkloof mjini Pretoria. Hata hivyo si wote waliopata nafasi ya kutoa heshima.
Mwanaharakati anayepigania haki za watu weusi nchini Marekani Jesse Jackson na kiongozi wa Ireland Sinn Fein Gerry Adams ni miongoni mwa viongozi wa kimataifa waliohudhuria hafla hiyo
Baadae jeneza la Mandela litachukuliwa kwa ndege kwenda katika kijiji cha Qunu katika jimbo la Cape ya Mashariki.
Jeneza hilo litasindikizwa na wanafamilia na maafisa wa serikali.
Hayati Mandela alifariki Decemba 5, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment