TANGAZO


Sunday, November 17, 2013

Watoto wenye mahitaji maalum wanahitaji kupata ulinzi na mapenzi ya mara kwa mara

Na Anna Nkinda – Colombo, Sri Lanka
WATOTO wenye mahitaji maalum wanahitaji kupata ulinzi na mapenzi ya mara kwa mara kutoka kwa walezi na jamii inayowazunguka ikiwa ni pamoja na kupata nafasi ya kwenda shule kwani wengi wao wananyimwa fursa hiyo  ukilinganisha na watoto wengine.

Aidha mtoto akipata elimu ni  moja ya hatua  ya mwanzo katika maendeleo ya taifa kwani  baada ya kuelimika atakuwa  na ujuzi wa kitaaluma, kiteknolojia na  raia mwenye kufuata maadili ya nchi yake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shule ya awali ya Carlton inayoongozwa na Mke wa Rais wa Sri Lanka Mama  Shiranthi Wickremasinghe Rajapaksa  wakati wake wa Marais na wakuu wa nchi na  Serikali walipotembelea shule hiyo iliyopo mjini Colombo jana ilionyesha kuwa shule hiyo inamtazamo wa  kutoa elimu kwa mtoto.

Elimu ya shule hiyo ambayo hutolewa bure kwa watoto wenye mahitaji maalum na wasio na mahitaji maalum imebuniwa kwa nia ya pekee ya kutoa elimu sambamba na viwango vya kimataifa kwa watoto wan chi hiyo ambao wanafundishwa kupitia njia rahisi ya nadharia na  vitendo ambavyo vinamfanya  mtoto aweze kuelewa zaidi.

Shule hiyo ilianza mwaka 1982 ikiwa na wanafunzi nane ambapo Mama Rajapaksa alikuwa ni mmoja wa walimu wawili waliokuwepo ambao waliweza kutoa elimu kwa watoto na kutokana na jitihada zake  baadhi yao baada ya kumaliza masomo wameweza kushika nyadhifa mbalimbali katika nchi hiyo  ikiwa ni pamoja na kuwakilisha Bunge la nchi.

Hasi sasa inamatawi nane yaliyopo katika mikoa mitatu ya nchi hiyo na kuwa na zaidi ya watoto 2000  huku ikiwa na malengo ya kuendeleza utu wa watoto, kutoa ujuzi wa uongozi, kuwawezesha watoto kuweza kujiamini na kujithamini, kukuza stadi za watoto, kusimamia  maadili na kurejesha nidhamu kwa watoto.

Walimu wa shule hiyo hufanya kazi ya kutambua vipaji vya watoto kwani huwapa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao katika matamasha ya mwisho wa mwaka na hivyo kuweza kutimiza ndoto zao na kupatikana kwa viongozi wazuri katika siku za usoni.

Wakiwa shuleni hapo wake hao wa marais na wakuu wa Serikali walijionea michezo mbalimbali iliyochezwa na watoto hao wenye umri wa chini ya miaka mitano ikiwemo ngoma, kareti na kuogelea ambayo inawajenga kiakili na kiafya na hivyo kuweza kufanya vizuri katika masomo yao.
Wake hao wa Marais na wakuu wa serikali  akiwemo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete walihudhuria mkutano wa 22 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) uliomalizika leo nchini humo.

No comments:

Post a Comment