Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano na Mfuko wa Pensheni wa PPF katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Hassan Silayo- MAELEZO)
Meneja Huduma kwa Wateja na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Godfrey Mollel akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), mpango wa mfuko huo kufikisha wanachama 400,000, ifikapo mwaka 2015 kwa sasa mfuko huo una wanachama takribani 300,000. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi. Lulu Mengele.
Na Hassan Silayo-Maelezo
Waajiri nchini wametakiwa kuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo elekezi kwa waajiriwa
kuhusu namna ya kujiandaa na maisha ya kustaafu tangu siku mfanyakazi
anapoingia katika ajira.
Wito huo umetolewa na meneja uhusiano na masoko wa mfuko wa pensheni wa
PPF Lulu mengele wakati wa mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika leo jijini dar es salaam.
Megele alisema kuwa kumekuwa na tabia ya waajiriwa
kusahau kujiwekea akiba na hivyo kusababisha matatizo wakati wa kustaafu.
”napenda kuwaasa waajiri waanzishe utaratibu wa
kutoa mafunzo elekezi kuhusu namna ya kujiandaa na maisha ya kustaafu tangu
siku mfanyakazi anapoingia katika ajira hii itamsaidia mfanyakazi kuwa na
mipango ya maandalizi kabla ya kustaafu na sio kusubiri mtu astaafu ndio aanze
kuweka mipango ya maisha yake”. Alisema Mengele.
Pia Menegele aliongeza kuwa kuna haja ya waajiri
nchini kuwapa fursa Wafanyakazi wapya kujiunga na Mifuko mbalimbali ya Hifadhi
ya Jamii.
“napenda kuwaasa waajiri wote nchini kuwapa fursa wafanayakazi
wapya kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwani kwa kufanya hivi kutaweza
kuwasaidia wafanyakazi kuwa na uwezo wa kujikimu na kukabiliana na changamoto
za maisha katika siku za baadae” alisema Mengele.
“kwasasa tuna wanachama 300,000 lakini kutokana na
ubora wa huduma za PPF tunategemea kuongeza idadi ya wanachama hadi kufikia 400,000
ifikapo mwaka 2015.
Mfuko wa pensheni wa PPF unajivunia kutekeleza
majukumu yake kwa asilimia 80 kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na
Mwasiliano (TEHAMA).
No comments:
Post a Comment