Kikundi cha ngoma cha Hengo, toka wilayani Kongwa, kikionesha umahiri wa kuimba na kucheza, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yanayofanyika kuanzia Nov 25 mpaka Des 10 2013, mkoani Dodoma.
Polisi wa kike waliopo kwenye kitengo maalumu cha Dawati la ukatili wa kijinsia wakiserebuka kwa wimbo wa wanawake na maendeleo, uliopigwa na kundi la FM Academia la jijini Dar es laam, wakati wa uzinduzi wa kupiga vita vitendo vya ukatili.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali, linalopiga vita vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, Sara Mwaga akifafanua jambo alipokuwa akisoma risala wakati wa uzindizi wa maadhimisho ya mpango huo. Kulia ni mgeni rasmi, Stephen Humbi na kushoto ni Mwakilishi wa Mkuu wa Magereza, ASP Shirima.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika uzinduzi huo, uliofanyika leo, katika Viwanja vya Nyerere, mjini Dodoma. (Picha zote na John Banda)
Unyanyasaji wa Kijinsia wakithiri Kanda ya Kati
Na John Banda, Dodoma
ASILIMIA %42 ya
kesi zilizoripotiwa polisi kwa kipindi cha miaka minne ni za vipigo kwa wanawake
hali inayodhoofisha afya jamii.
Takwimu hiyo
iliyotolewa wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia
kanda ya kati ilitolewa na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserekali
linalopinga ukatili wa kijinsia na watoto [AFNET] Bi Sara Mwaga.
Mkurugenzi huyo
alisema kesi zinazoongoza kupokelewa na jeshi la polisi mkoani hapa ni za vipigo
hasa kwa wanawake vinavyofanywa na wenzi wao katika ndoa na walio katika
mahusiano ya kimapenzi.
‘’Bi Sara
alisema kuwa kesi za vipigo zinaongoza kwa asilimia 42, ikifuatiwa na Ubakaji
32.7%, Shamburio la mwili lenye 16.9% wakati vitendo vya ulawiti
ni 7.4.5. ambapo umepungua toka %15 ya mwaka 2012 hali hii inadhoofisha afya ya
jamii’’, alisema
Aidha alisema
pamoja na takwimu kuonyesha tatizo la ukatili wa kijinsia kuwa juu kitakwimu
lakini hali halisi ni mbaya zaidi kuliko invyoonekana kutokana na kesi chache
sana zinazoripotiwa kwenye vyombo vya dola hadi hivi sasa.
Alisema pamoja
na hilo ni kesi chache kati hizo zinazoripotiwa zinazofikia mwisho na wahusika
kuchukuliwa hatua zinazosihili, huku akibainisha kuwa tatizo ni watu kutoelewa
haki zao na nini cha kufanya ili kuzidai.
Uzindizi wa
Maadhimisho hayo yanayofanyika kwa siku 16 katika ukanda wa kati unashirikisha
mikoa iliyoathirika kwa kiasi kikubwa na tatizo hilo la unyanyasaji na ukatili
wa kijinsia ya Singida, Tabora na Dodoma.
No comments:
Post a Comment