TANGAZO


Wednesday, November 20, 2013

SSRA yatoa miongozo Sita ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii



Na Fatma Salum-MAELEZO
Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA) Imetoa miongozo sita (6) kwa lengo la kuhakikisha sekta ya hifadhi ya Jamii Inakuwa bora na endelevu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa mamlaka hiyo Sarah Kibonde wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari, leo Jijini Dar es Salaam.

Sarah alisema kuwa miongozo hiyo itakayo boresha maisha ya wanachama na kuchangia maendeleo ya nchi kwa ujumla ni pamoja na muongozo wa uandikishaji wa wanachama,uwekezaji,takwimu,utawala bora wa bodi za wadhamini,tathmini  za Mifuko na kujumlisha vipindi va michango.

“Mamlaka imetoa miongozo hii ili kutekeleza jukumu lake la kulinda,kutetea na kuendeleza maslahi ya wanachama wa sekta ya hifadhi ya jamii kama ilivyoainishwa kwenye sheria iliyounda mamlaka hii”. Alisema Sarah.

Aidha Sarah alifafanua kuwa miongozo hiyo pia itasaidia kuhakikisha mwanachama anapata haki yake anayostahili kwa wakati muafaka na kuondoa migongano baina ya mifuko,waajiri na waajiriwa.

Pia Miongozo hiyo itahakikisha uwekezaji wa mifuko unaleta maendeleo bila kuhatarisha afya ya mifuko na utawala bora unazingatiwa katika shughuli zote za uwekezaji kwa manufaa ya mifuko,wanachana na Taifa kwa Ujumla.

Mamlaka inategemea kuwa katika kipindi cha miaka 5 ijayo sekta ya hifadhi ya jamii itakuwa endelevu,yenye mafao bora na mifuko ya hifadhi ya jamii itaongezeka.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji toka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah kibonde akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo, jijini Dar es Salaam, juu ya miongozo sita inayolenga kuhakikisha sekta ya hifadhi ya jamii inakuwa bora na endelevu. Kulia ni Mkurugenzi wa Sheria toka Mamlaka hiyo Bwana Ngabo Ibrahim.
Mkurugenzi wa Sheria toka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bwana Ngabo Ibrahim akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo, jijini Dar es Salaam, vigezo vya kuzingatia kwa makampuni na wataalam wanaotarajia kufanya tathmini za mifuko.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na uhamasishaji toka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah kibonde (hayupo  pichani) leo, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Eliphace Marwa-MAELEZO)

No comments:

Post a Comment