Mahakama, nchini Tanzania imetupilia mbali ombi la kusikilizwa
upya kwa kesi dhidi ya muimbaji Nguza Viking, anayejulikana kama Babu Seya
pamoja na mwanawe, ambao walihukumiwa maisha jela, kwa kosa la ubakaji.
Majaji walisema kua kuna thibitisho tosha kuwa wawili hao waliwabaka watoto
10 wa shule ya msingi mwaka 2013.Kesi hiyo imewashtua mashabiki wa Viking katika nchi hiyo iliyo katika kanda nzima ya Afrika Mashariki.
Mwanamuziki huyo mwenye kuimba nyimbo za Rhumba, ambaye ni mzaliwa wa DRC, ameishi Tanzania kwa miaka mingi na kuwa na ufuasi mkubwa huko.
Mwandishi wa BBC Ben Mwang'onda mjini Dar es Salaam anasema kuwa Viking na kijana wake Johnson Nguza ambaye pia ni mwanamuziki, walifika mahakamani kwa uamuzi huo.
Walionekana kuwa watulivu wakati majaji walipotupilia mbali ombi lao kutaka hukumu yao kubatilishwa.
Walihukumiwa kwa kuwabaka wasichana 10 wa shule ya msingi waliokuwa kati ya umri wa miaka sita na nane wote waliokuwa katika shule ya msingi ya Mashujaa mtaani Kinondoni mjini Dar es Salaam.
Wakili wa muimbaji huyo alisema kua muimbaji huyo hana matumaini tena ya kupewa rufaa kwani hili ndio lilikuwa ombi lake la mwisho.
No comments:
Post a Comment