Shirika la Taifa la hifadhi ya jamii (NSSF)
linaendelea na mikakati wa kutatua changamoto za makazi kwa wanachama wake.
Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano na Huduma kwa
Wateja wa shirika hilo Eunice Chiume wakati wa mkutano na waandishi wa habari
leo Jijini Dar es Salaam.
Eunice alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa hitaji kubwa ya makazi shirika limejipanga kukabiliana
na changamoto hiyo kwa kuendelea kujenga nyumba za bei nafuu zitakazouzwa kwa
wanachama wake ili kuweza kuwapatia makazi ya kudumu.
“baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza naya pili
ya ujenzi wa nyumba 297, NSSF tumeona kuna haja ya kuendelea kukukabiliana na
hali hii kwa kuanzisha awamu ya tatu ya mradi wa nyumba za bei nafuu
itakayohusisha ujenzi wa nyumba 900 zitakazogharimu takriban shilingi bilioni 23.” alisema Eunice.Aidha Eunice aliongeza kuwa kuanzia November 11 mwaka huu Shirika linatarajia kuanza kutoa fomu za maombi ya kununua viwanja 498 vilivyopimwa katika eneo la kiluvya A madukani, viwanja hivyo vitauzwa kwa ushirikiano wa shirika na Halmashauri ya wilaya ya kisarawe, ambapo eneo hilo litakuwa makazi mapya nay a kisasa litakalokuwa na huduma muhimu za kijamii.
Viwanja hivyo vitauzwa kwa wanachama wa NSSF na jamii kwa ujumla kwa bei inayoanzia Shilingi 15,000 hadi Shilingi 20,000 kwa mita ya mraba kulingana na matumizi.


No comments:
Post a Comment