TANGAZO


Tuesday, November 12, 2013

Nabii adaiwa kubaka mwanafunzi Dodoma na kumtia mimba

Na John Banda, Dodoma

NABII Elisha Muliri wa kanisa la Ebeneza mjini Dodoma, ameingia matatani baada ya kudaiwa kumbaka na kumtia mimba mwanafunzi na kukatiza masomo yake huku kutishia kumuua.

Akisimulia tukio hilo, mbele ya waandishi wa habari, mwanafunzi huyo (jina tunalihifadhi) wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya City iliyopo manispaa ya Dodoma, alisema kuwa kabla ya kufanyiwa kitendo hicho, alikuwa anaangushwa na mapepo.

Alisema baada ya kuhangaika kwa muda mrefu bila mafanikio, walipata taarifa za ujio wa nabii huyo, mjini humo na wapofika ili kupata msaada wa kuombewa mapepo hayo, yalilipuka na binti akaponywa hata leo na kuahidiwa mbele ya kanisa kusaidiwa ada na Nabii huyo.

Binti huyo, alisema baada ya kuponywa akaendelea kwenda kusali kanisani hapo ambapo kutokana na kila mtu anayefika na kufanyiwa maombi huacha mawasiliono kwenye vikaratasi, na Juni 8 mwaka huu, akapigiwa simu na nabii huyo, akipewa maelekezo ya kufika nyuma ya ukumbi wa Paradise, ambapo walikuwa wakifanyia ibada.

Anatanabahisha kuwa baada ya kuonana nabii, alimwambia aingie kwenye gari, akaingia akifikiri kuna heri, akapewa soda aina ya Fanta orange, alipokunywa akapoteza fahamu na alipokuja kuzinduka alijikuta akiwa nyumba za kulala wageni Makole na nabii akiwa amemlalia kama alivyozaliwa, huku akiangalia mkanda wa ngono.

‘’Wakati nataka kupiga kelele, alinitishia kwamba ataniua kama nitathubutu kumwambia mtu yoyote jambo hilo, akanipiga kofi na kuniambia yeye hawezi kunilipia ada bure kwa sababu mimi siyo ndugu yake, lazima lazima alale na mimi mara 5, kwa hiyo, bado mara 4 na kunisisitiza, asisikie popote kuwa alinifanyia hivyo’’, alisema mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake, mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Mary Mkombora, alisema alimpeleka kuombewa kutokana na kusubuliwa na mapepo tangu akiwa darasa la sita na wakakubaliana na nabii huyo, kumlipia ada kwa awamu, hivyo akachukue 50,000, kila mwezi ili kukamilisha 400,000, inayotakiwa shule.

"Nilimgundua yupo tofauti kuanzia mwezi wa saba, nilipomuuliza alisema yeye haelewi, siku moja nikamshuhudia akitapika asubuhi, ndipo nilipomchapa na kumfukuza, nikapigiwa simu na waliompokea kuwa mtoto kapewa mimba hiyo na nabii, kwanini nimemfukuza, ndipo nikachoka, alipopimwa alikuwa na mimba", alisema.

Aliongeza kuwa nabii huyo, ambaye alikuwa mume wa mwimbaji marufu wa nyimbo za Injili, marehemu Anjela Chibalonza kwa sasa hajulikani alipo, japo mara kadha wasaidizi wa kanisa hilo, ambalo limebadilishwa jina kutoka Shakinah Pentecostal Church na kuitwa Ebeneza amekuwa akitaka Suluhu.

 ‘’sasa hivi mimi na mtoto wangu tumekuwa tukiishi mashakani baada ya Msaidizi wake, nabii Monica, nimpe huyo binti (akamtaja jina), akamtoe mimba kwa wataalamu wanaowajua wao, siku ambayo alichukua kadi yenye namba za simu na kufuta meseji zote mwanangu alizokuwa akiandikiwa na nabii huyo,’’ alisema.

Nabii huyo kwa sasa hajulikani alipo na hata alipotafutwa kwa simu yake ya mkono 0756 409118, ilikuwa amezimwa na msaidizi wake, nabii Monica Nyambura, raia wa Kenya, anakotokea Elisha Muliri, alisema yeye hawezi kuongelea jambo hilo kwakua yeye ni mgeni ameachiwa kanisa hilo baada ya mwenyeji wake kuwa safarini hivyo, asubiriwe mwenyewe kwani hatachelewa.

Tukio hilo, limefikishwa katika kituo cha sharia cha Tanzania Legal Centre [TALAC] na mwanasheria mfawidhi mkazi Dodoma Godwin Ngongi tayari ameshamuandikia mkuu wa kituo cha Polisi cha Kati, barua ya kuwataka kumkamata mtuhumiwa huyo, ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria na pia kuepusha  mwanfunzi huyo na hatari nyingine.

Jeshi hilo, limekiri kuwa na taarifa ya tukio hilo na kwamba wanaendelea na uchunguzi.
                                               

No comments:

Post a Comment