Habari zilizotufikia hivi punde, zinasema kwamba Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Sengodo Mvungi (pichani), amefariki dunia katika Hospitali ya MillPark huko nchini Afrika Kusini alikokuwa akipata matibabu baada ya kupugwa mapanga na wanaodhaniwa kuwa majambazi nyumbani kwake, Kibamba Msakuzi hivi karibuni na kisha kupelekwa nchini humo kwa matibabu zaidi.
Dk. Mvungi alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Oktoba 2, mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.
Mauti yamemkuta mnamo majira ya saa tisa na nusu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema, Peponi.
Mtandao wa bayana kwa kushirikiana na vyombo vyengine vya habari, unatoa pole kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, familia, ndugu na jamaa pamoja na Chama chake cha NCCR-Mageuzi kwa msiba huo pamoja na Watanzania wote kwa ujumla. (Habari na picha kwa hisani ya MO blog)
No comments:
Post a Comment