Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa Dernmark, Margrethe Vestager, walipokutana kujadili mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya uchumi katika kikao kilichofanyika katika mji wa Copenhagen nchini Denmark.
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchu (CUF, Profbrahim Lipumba alikutamamkutana na Naibu waziri mkuu wa Dernmark Bi. Margrethe Vestager kujadili mambo mbalimbali ikiwemo uchumi katika kikao kilichofanyika katika mji wa Copenhagen nchini Denmark.
Katika mazungumzo hayo walijdaili
matatizo ya uchumi yanayokabila nchi za Ulaya hasa ukanda wa Euro vinavyoathiri
nchi za Afrika ikiwemo Tanzania na hatua za kuchukua.
Mambo mengine yaliyogubiga mzungumzo
hayo ni pamoja na tatizo la ajira kwa vijana ulimwenguni, Misaada ya Maendeleo
kwa nchi maskini na ujenzi wa uhusiano mzuri kati ya CUF na chama cha Radikale
Venstre.
Bi. Margrethe Vestager ambaye ni kiongozi
wa Chama cha Radikale Venstre pia ni Naibu Waziri Mkuu katika Seikali ya Mseto
ya Denmark inayojumlisha vyama vitatu vya Social Democrats, Radicale Venstre na
Socialist People Party.
Majadiliano hayo yalifanyika wakati
wa ziara ya ujumbe wa CUF Denmark kwa mwaliko wa chama cha Radicale Venstre.Ujumbe
wa CUF ulijumuisha viongozi mbalimbali wa chama pamoja na wanachama uliofanyika
kuanzia terhe 26Oktoba 2013 mpaka 3 Novemba 2013.
Imetolewa na
Abdual
KambayaImetolewa na
Naibu Mkurugenzi wa Haki za binadamu , sheria na Habari CUF
0719566567


No comments:
Post a Comment